Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool kuendelea kumlipa Diogo Jota

Muktasari:

  • Jota, 28 na mdogo wake Silva walitangazwa kufariki dunia baada ya timu ya waokoaji ilipokwenda kwenye eneo la ajali asubuhi ya Alhamisi iliyopita.

LISBON, URENO: WAKATI dunia ya wanasoka ikiendelea kuombeleza kifo cha mchezaji Diogo Jota, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari akiwa na mdogo wake, Andre Silva, klabu yake ya Liverpool imefunguka itaendelea kuilipa familia yake kwa muda uliobaki wa mkataba wake katika kikosi hicho cha Anfield.

Jota, 28 na mdogo wake Silva walitangazwa kufariki dunia baada ya timu ya waokoaji ilipokwenda kwenye eneo la ajali asubuhi ya Alhamisi iliyopita.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Ureno, Jota alishauriwa na madaktari wake asitumie usafiri wa anga baada ya kufanyiwa upasuaji wa mapafu.

Katika kuonyesha kuumizwa na jambo hilo, Liverpool imekubali kuilipa familia ya Jota, ambaye ni mkewe na watoto wa tatu sehemu yote ya mkataba ya mchezaji huyo ambayo imebaki.

Mke wa Jota, mrembo Rute Cardoso, ambaye alifunga pingu za maisha na kipenzi chake hicho cha moyo tangu utotoni wiki mbili tu zilizopita kabla ya kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha.

Jota, ambaye aliitumikia Liverpool kwenye mechi 182 tangu alipojiunga akitokea Wolverhampton Wanderers, alikuwa akilipwa mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki huko Anfield.

Kwa mujibu wa gazeti la Ureno, Record, inaripoti Liverpool itaendelea kulipa mshahara huo hadi mwisho wa mkataba wa Jota.

Hiyo ina maana, kiasi cha Pauni 14,560,000 kitalipwa hadi hapo mkataba wake utakapofika tamati wakati wa dirisha la majira ya kiangazi 2027.

Si jambo hilo tu, lakini mabosi wa Anfield wamefanya uamuzi wa kuipa umuhimu mkubwa jezi Namba 20, ambayo iliyokuwa ikivaliwa na Jota kwa kipindi cha misimu mitano mfululizo.

Jota, baada ya kuisaidia Wolves kupanda daraja kucheza Ligi Kuu England, alijiunga na Liverpool wakati wa dirisha la majira ya kiangazi 2020 na haraka akawa mchezaji muhimu kikosini.

Mabosi wa Liverpool, Michael Edwards na Richard Hughes walifichua na kuahidi kwamba watafanya tukio la kusherehekea jezi Namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na mkali huyo wa Ureno.