Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakala wa Tonali aiamsha Arsenal

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Italia mwenye thamani ya Pauni 100 milioni, umri wa miaka 25, amekuwa gumzo kubwa wiki hii huku Arsenal, Manchester City na Chelsea zote zikionyesha nia ya kumsajili, pamoja na klabu kadhaa za Serie A.

NEWCASTLE, ENGLAND: WAKALA wa kiungo Sandro Tonali ameiamsha Arsenal akidai kwamba anapanga kufanya mazungumzo na Newcastle United majira ya kiangazi kuhusu mustakabali wa nyota huyo.

Kiungo huyo wa Italia mwenye thamani ya Pauni 100 milioni, umri wa miaka 25, amekuwa gumzo kubwa wiki hii huku Arsenal, Manchester City na Chelsea zote zikionyesha nia ya kumsajili, pamoja na klabu kadhaa za Serie A.

Sun Sport ilifichua jinsi Tonali hakuficha kabisa kufadhaika kwake kufuatia mfululizo wa ushindi mmoja tu katika mechi saba, alipokuwa akipita mbele ya waandishi wa habari katika eneo la mahojiano (mixed zone) baada ya kipigo cha Carabao Cup dhidi ya Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad, Jumatano iliyopita.

Hilo lilitokea chini ya saa moja baada ya kubadilishana maneno hadharani uwanjani na kocha wa Man City, Pep Guardiola, tukio lililoibua mjadala mkubwa. Kocha wake Eddie Howe alifanya mazungumzo na Tonali wiki hii na kusisitiza kuwa kiungo huyo alimthibitishia kuwa ana furaha kuendelea kubaki Tyneside.

Wakala wa mchezaji huyo, Giuseppe Riso, pia alikanusha ripoti zilizodai kuwa aliwasiliana na Arsenal siku ya mwisho ya dirisha la usajili kuhusu dili linalowezekana jambo ambalo viongozi wa Newcastle wanaamini lilitokea.

Riso alisema: “Newcastle wanapata ugumu kumuacha Sandro, na yeye anataka kuiongoza klabu kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mazungumzo haya ya uhamisho yatafanyika baadaye. Tutaona msimu utakavyomalizika kisha tutaamua nini cha kufanya. Kwa sasa hakuna upendeleo wowote. Bado ni mapema. Tunachosema leo huenda kisihusike kesho. Newcastle wasingeweza kumuacha aondoke sasa, na hakuna maana ya kuhama, hasa kwa kuwa Sandro ana mapenzi makubwa na klabu. Tutatathmini na kuamua majira ya kiangazi.”

Tonali, ambaye mwezi uliopita yeye na mke wake Juliette walipata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Leonardo, ana uhusiano wa karibu na Howe na anaendelea kuishukuru klabu kwa kumuunga mkono wakati wa kifungo chake cha miezi kumi kutokana na kesi ya kubeti. Staa huyo analipwa Pauni 150,000 kwa wiki huku mkataba wake utafika ukomo 2029.