Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakala wa Gyokeres kutua London

WAKALA Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa tovuti ya GMS sources, wakala huyo ataanza kukutana na Arsenal ambao ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili Gyokeres kwa sasa.

LONDON, ENGLAND: WAKALA wa mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Victor Gyokeres anatarajiwa kutua London, mwezi ujao kufanya mazungumzo na baadhi ya timu zinazohitaji huduma ya mchezaji wake.

Kwa mujibu wa tovuti ya GMS sources, wakala huyo ataanza kukutana na Arsenal ambao ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili Gyokeres kwa sasa.

Mbali ya Arsenal, pia atazungumza na baadhi ya wawakilishi wa timu nyingine ikiwemo Manchester United iliyokuwa ikihusishwa naye tangu mwaka jana.

Inaelezwa timu zote zipo tayari kutoa kiasi cha Pauni 70 milioni kinachohitajika na Lisbon ili kumuuza fundi huyu na kinachokwamisha dili kwa sasa ni makubaliano binafsi baina ya timu hizo na wawakilishi wa Gyokeres.

Kwa mujibu wa ripoti, Gyokeres ambaye kwa sasa analipwa mshahara wa Pauni 640,00 kwa wiki, anataka mshahara ambao utakuwa ni mara tatu ya sasa kiasi ambacho timu hizo zipo tayari kutoa.

Arsenal inadaiwa kutaka kutoa pesa nyingi zaidi ya hizo ambazo fundi huyu anahitaji kama mshahara ikiwa ni katika njia mojawapo ya kuwazidi kete wapinzani wao.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na fundi huyu ambaye msimu huu amecheza mechi 48 za michuano yote na kufunga mabao 52, hataki kufanya maamuzi ya kukurupuka na anataka kufikiria kwa muda na kutazama uzito wa kila ofa kabla ya kuamua ni timu ipi atajiunga nayo.

Timu nyingi zinamtolea macho staa huyu baada ya Newcastle kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kumuuza straika wao Alexander Isak.