Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yakwaa kisiki CAS, TPLB kutangaza ratiba mpya ya ligi punde

Muktasari:

  • Yanga iliwasilisha CAS madai kuhusiana na kutoridhishwa kuahirishwa kwa mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa Machi 8, 2025.

MAKAHAMA ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imeitupa rufani ya Klabu ya Yanga iliyofungua dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga iliwasilisha CAS madai kuhusiana na kutoridhishwa kuahirishwa kwa mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa Machi 8, 2025.

Walalamikiwa wengine katika shauri hilo ni Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Klabu ya Simba ambapo pamoja na mengine, Klabu ya Yanga iliomba mechi hiyo isipangwe tarehe mpaka litakapotolewa uamuzi.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) leo Mei 1, 2025, imeeleza kuwa: "Kutokana na uamuzi huo wa CAS, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inaendelea na maandalizi yake ya kuhitimisha msimu wa Ligi Kuu 2024/2025 na kufanya maboresho ya ratiba ya ligi ukiwemo mchezo namba 184, Yanga vs Simba kisha kutangaza ratiba mpya mapema iwezekanavyo."

Ikumbukwe kuwa, kabla ya kuahirishwa mchezo huo,  Simba iliiandikia Bodi ya Ligi kutokuwa tayari kucheza kufuatia kunyimwa haki yao kikanuni ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi.

Bodi ya Ligi iliridhia suala hilo na kuahirisha mchezo huo jambo ambalo Yanga haikukubaliana nalo na kwenda CAS kufungua shauri ikihitaji kupatiwa pointi tatu kwa kile walichodai kanuni zilikiukwa.