Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viungo wanasakwa Manchester United

Muktasari:

  • Man United imekuwa ikifuatilia viungo wenye vipaji vikubwa kwenye Ligi Kuu England, Elliot Anderson, Adam Wharton, Carlos Baleba na Alex Scott katika mchakato wao wa kujitengeneza kwenye eneo hilo la katikati ya uwanja.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inajiandaa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kusajili pacha mpya ya safu ya kiungo wakati wa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Man United imekuwa ikifuatilia viungo wenye vipaji vikubwa kwenye Ligi Kuu England, Elliot Anderson, Adam Wharton, Carlos Baleba na Alex Scott katika mchakato wao wa kujitengeneza kwenye eneo hilo la katikati ya uwanja.

Bruno Fernandes anaibua wasiwasi juu ya hatima yake kwenye kikosi cha Man United kutokana na kile alichokizungumza hivi karibuni, huku viungo wenzake nao Kobbie Mainoo, Casemiro na Manuel Ugarte wakiwa kwenye wasiwasi mkubwa.

Katika mahojiano aliyofanya mwezi uliopita kupitia Shirikisho la Soka la Ureno, Fernandes, ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, alidai Man United ilitaka kumuuza dirisha lililopita la majira ya kiangazi na kubainisha mpango wake ni kucheza Ureno au Italia.

Man United iligomea ombi la Mainoo la kutaka kuondoka kwa mkopo dirisha lililopita la majira ya kiangazi na huenda akalazimisha uhamisho kwenye dirisha la Januari kama hatapewa muda wa kucheza.

Casemiro, ambaye atatimiza umri wa miaka 34 Februari mwakani, mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu na kuna uwezekano akaruhusiwa kuondoka.

Ugarte, ambaye alijiunga na Man United kwa ada ya Pauni 50.75 milioni na ameanzishwa kwenye mechi nne tu msimu huu na zote hizo miamba hiyo ya Old Trafford ilikumbana na kichapo.

Man United ilifanya majaribio ya kutaka kumsajili kiungo wa Brighton, Baleba kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi wakati alipoona kama Ugarte kiwango chake kimekuwa na mushkeli mkubwa kwenye Ligi Kuu England.

Fernandes na Casemiro kwa sasa ndiyo wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwenye kikosi cha Man United na kama Marcus Rashford na Jadon Sancho wataondoka jumla jambo hilo litaifanya timu hiyo kuwa na pesa ya ziada ya kuwekeza kwenye kikosi chao. Man United imesajili viungo wawili tu wa kati, Casemiro na Ugarte katika kipindi cha miaka saba.

Miamba hiyo ya Old Trafford ilishindwa kumsajili Declan Rice kutoka West Ham United kabla ya kujiunga na Arsenal kwa ada ya Pauni 105 milioni mwaka 2023 licha ya kwamba Rice alikuwa tayari kujiunga na Man United.

Kiungo wa Nottingham Forest, Anderson, 23, bado ana mkataba na miamba hiyo ya City Ground hadi 2029 na thamani yake imepanda tangu alipoanza kupata nafasi kwenye kikosi cha England chini ya kocha Thomas Tuchel. Forest ilimsajili Anderson kwa ada ya Pauni 35 milioni kutoka Newcastle United miezi 18 iliyopita.

Wharton, 21, ambaye yupo kwenye bei zinazoweza kufikiwa na Man United yupo kwenye timu ya Crystal Palace, ambayo huwa haijawahi kuwa na woga wa kuwapiga bei mastaa wake. Michael Olise aliuzwa kwa Pauni 50.8 milioni kwenda Bayern Munich mwaka jana na Arsenal ilimsajili Eberchi Eze kwa Pauni 60 milioni kwenye dirisha lililopita.

Mkataba wa Wharton nao utafika tamati 2029 na anafikiria kusaini dili jipya.

Kiungo Baleba, 21, ana mkataba Brighton hadi 2028, lakini Mcamerooni huyo ndoto zake ni kwenda Man United.

Kuhusu Scott, 22, naye amekuwa kwenye kiwango bora Bournemouth na ndiyo maana Man United inahitaji huduma yake.