Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yavamia winga Sauzi! Ni yule aliyezungumza na Yanga


SIMBA inaendelea kujenga timu kwa hesabu za msimu ujao ambapo baada ya kupata kiungo mkabaji sasa iko mezani na winga mmoja wa kushoto ambaye jina lake sio geni pale Yanga.


Mabosi wa Simba wanafanya mazungumzo na winga wa kushoto Keletso Makgalwa ambaye amemaliza msimu wa 2025-2026 akiitumikia Shekhukhune ya Afrika Kusini.

Makgalwa ni winga fundi ambaye anatumia mguu wa kulia lakini anapenda kushambulia akitokea kushoto akiwa na kasi kubwa na ujuzi wa kujua kuwapangua mabeki.

Winga huyo ni mmoja ya wachezaji waliopendekezwa na kocha Steve Barker akitaka kuongeza mtu mwingine bora wa kujua kufungua ukuta wa wapinzani.

Kwenye ripoti ya msimu uliomalizika, Barker ameonyesha kama Simba ikimkosa winga wake mmoja kati ya Anicet Oura au Libase Gueye, inakabiliana na changamoto ya kujenga mashambulizi kutokea pembeni.

Barker alitoa mfano ilivyotokea kwenye mchezo dhidi ya Yanga pale Uwanja wa New Amaan Zanzibar kwenye fainali ya Kombe la Muungano ambapo baada ya kuumia Oura, Wekundu hao wa Msimbazi hawakuwa na mashine nyingine kama winga huyo raia wa Ivory Coast.

Simba bado inapambana na Makgalwa kwenye mazungumzo hayo yanayofanywa na bosi mmoja wa juu kwenye bodi ya klabu hiyo, akitaka kufunga dili hilo mapema.

Msimu uliomalizika Makgalwa alikuwa kwenye kiwango bora akihusika kwenye mabao nane akifunga mawili na kutengeneza asisti sita.

"Bado tunaendelea na mazungumzo hatujafikia mwisho, ila muafaka utapatikana, huyu ni mchezaji ambaye amependekezwa na kocha mwenyewe kwani anamjua vizuri kwa kuwa alikuwa anamuona huko Afrika Kusini," alisema bosi huyo.

"Tuna machaguo mengi kwenye kila nafasi ambayo tunataka kutafuta wachezaji wapya, kuna watu wawili mpaka watatu, kwahiyo tunapambana.

"Tunataka kumaliza hii kazi mapema ili tuanze mapema maandalizi, tuna wiki chache sana za kukamilisha masuala ya usajili ili tuanze kujipanga na msimu ujao."

Makgalwa aliwahi kufanya mazungumzo na Yanga msimu uliomalizika lakini Shekhukhune ikagoma kumuachia kisha kuchukuliwa mshambuliaji Andy Boyeli kwa mkopo ambaye naye hata hivyo hakuweza kufanya makubwa.