Vita imerudi upyaa langalanga

Muktasari:
- Ni katika mbio 12 za kwanza zilizopita, kumeshuhudiwa washindi saba tofauti wakiibuka na ushindi wa mbio tofauti na kuifanya mbio iwe na msisimko wa aina yake mwaka huu tofauti na misimu miwili iliyopita.
ULE utamu wa mbio za magari duniani (Formula One) unarudi tena wikiendi hii baada ya kusimama kwa mapumziko ya duru la kwanza la msimu mzima wa mbio hizo.
Ni katika mbio 12 za kwanza zilizopita, kumeshuhudiwa washindi saba tofauti wakiibuka na ushindi wa mbio tofauti na kuifanya mbio iwe na msisimko wa aina yake mwaka huu tofauti na misimu miwili iliyopita.
Mbio mbili za mwisho, England na Ubelgiji mshindi alikua ni Lewis Hamilton wa Mercedes ambaye amerudi kwenye makali yake na kumpa presha bingwa mara tatu mfululizo, Max Verstappen wa Red Bull ambaye ana kazi ya kutetea ubingwa huo kupitia mbio 10 zijazo.
Hadi sasa, Verstappen anaongoza kwa pointi 277, Lando Norris wa McLaren ana 199, Charles Leclerc wa Ferrari 177, Oscar Piastri wa McLaren 167, Carlos Sainz wa Ferrari 162, Hamilton 150, Sergio Perez wa Red Bull 131, George Russell wa Mercedes 116, Fernando Alonso 49 na Lance Stroll akifunga 10 bora kwa pointi 24.