Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hata Ahoua, Mzize wana kazi nzito

KAGERA Pict

YANGA imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu 2024/25 likiwa ni taji la 31 tangu kuasisiwa kwa ligi hiyo mwaka 1965, ambalo limetua mitaa ya Jangwani na Twiga baada ya kulisotea kwa muda msimu huu kutokana na danadana nyingi hapo kati zilizosababisha ile ya Dabi ya Kariakoo kuahirishwa mara mbili.


Hata hivyo, kuna mengi matamu yaliyoibuka msimu huu yakiambatana na mshikemshike wa michuano ya Ligi Kuu Bara ambayo kwa mashabiki wengi walikuwa wakitega masikio kufuatilia viwanjani na kwenye runinga kuona kilichokuwa kinajiri, huku kukiwa na mambo flani ya kusisimua.


Lakini wakati ligi ikifikia mwishoni, rekodi ya nyota wa zamani wa Simba anayekipiga Namungo, Meddie Kagere ‘MK 14’ a.k.a The Terminator inaendelea kuwatesa mastaa Ligi Kuu.

Nyota huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya ndiye mchezaji pekee aliyewahi kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora na kuitetea na tangu afanye hivvo misimu sita iliyopita, hakuna mwingine aliyeifikia hadi sasa.

Kagere aliyetua nchini kujiunga na Simba akitokea Gor Mahia 2018-2019 alifunga mabao 23 na kuwa nyota wa kwanza wa kigeni kufunga mabao mengi akiipiku rekodi ya mabao 21 iliyokuwa ikishikiliwa n Amissi Tambwe akiwa na Yanga 2015-2016.

Nyota huyo wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, alitetea tuzo hiyo msimu uliofuata 2019-2020 kwa mabao 22 na kuandika rekodi nyingine mpya ya mchezaji wa kwanza kutetea tuzo hiyo, kwani haikuwahi kutokea kwa wazawa au kigeni.

KAGERA Pict

Hata hivyo, tangu Kagere afanye hivyo hakuna mchezaji mwingine aliyefikia rekodi hiyo na hata yeye mwenyewe hajatwaa tena tuzo na badala yake mastaa wa timu tofauti wanatwaa na kutema huku wageni wakitawala kulinganisha na wazawa.

John Bocco aliyewahi kutamba Azam na Simba kabla ya msimu huu kukipiga JKT Tanzania, Simon Msuva na Tambwe wamewahi kutwaa tuzo ya mara mbili, lakini kwa misimu tofauti kulinganisha na Kagere aliyebeba back to back. 

Bocco alitwaa ya kwanza 2011-2012 akiwa Azam akifunga mabao 19 na kuibeba tena 2020-2021 akiitumikia Simba alipofunga 16, wakati Tambwe alibeba 2013-2014 akiwa Simba kwa mabao 19 na kutwaa tena 2015-2016 akiichezea Yanga akiifunga 21, ilihali Msuva alibeba 2014-2015 kwa mabao 17 na kurudia 2016-2017 alipofunga 14 akilingana na Abdulrahman Mussa aliyekuwa Ruvu Shooting. Tangu Kagere alipotwaa mara mbili mfululizo, hakuna mchezaji aliyewahi kurudia.

Kabla ya Kagere kubeba tuzo hizo mara mbili kuanzia 2004 rekodi zinaonyesha Mfungaji Bora alibeba tuzo mara moja na kushindwa kuitetea msimu uliopita na kuonyesha Mnyarwanda huyo bado hajatafutiwa dawa licha ya mastaa wenye majina kuja na kuondoka.

Kwa msimu huu, Kagere amemaliza na mabao mawili aliyoyafunga katika mechi ya mwisho dhidi ya KenGold wakati Namungo ikishinda 5-0 na kumfanya aboreshe hazina yake ya kutupia tangu aanze kuichezea ligi hiyo akifikisha 77.

Mabao aliyofunga katika misimu saba kupitia Simba, Singida Fountain Gate na Namungo yamemfanya Kagere awe nyota wa kigeni mwenye mabao mengi akiipiku rekodi ya Tambwe ya kufunga mabao 75 kupitia misimu saba pia akiwa na Simba, Yanga na Singida Big Stars.

ORODHA WAFUNGAJI BARA TANGU 2004-2025
2004- Abubakar Mkangwa (Mtibwa Sugar, 16)
2005 - Isse Abshir (Simba, 19)
2006- Abdallah Juma (Mtibwa Sugar, 25)
2007/08 Michael Katende (Kagera Sugar, 11)
2008/09 Boniface Ambani (Yanga, 18)
2009/10 Mussa Mgosi (Simba, 18)
2010/11 Mrisho Ngassa (Azam, 18)
2011/12 John Bocco  (Azam, 19)
2012/13 Kipre Tchetche (Azam, 17)
2013/14 Amissi Tambwe (Simba, 19)
2014/15 Simon Msuva (Yanga, 17)
2015/16 Amissi Tambwe (Yanga, 21)
2016/17 Simon Msuva (Yanga, 14) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting, 14)
2017/18 Emmanuel Okwi (Simba, 20)
2018/19 Meddie Kagere (Simba, 23)
2019/20 Meddie Kagere (Simba, 22)
2020/21 John Bocco (Simba, 16)
2021/22 George Mpole (Geita Gold, 17)
2022/23 Fiston Mayele (Yanga, 17) na Saido Ntibazonkiza (Geita/ Simba, 17)
2023/24- Stephane Aziz KI (Yanga, 21)
2024-25- Jean Charles Ahoua (Simba, 16)