Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ataka aletewe msaidizi

Muktasari:

  • Kocha huyo Mreno anataka kuimarisha benchi lake la ufundi ili yasijirudie ya msimu uliopita wakati timu hiyo ilipofanya hovyo na kumaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amewaomba mabosi kufanya kila wanaloweza ili kumletea msaidizi wake wa zamani Acacio Valentim  wapige mzigo Old Trafford.

Kocha huyo Mreno anataka kuimarisha benchi lake la ufundi ili yasijirudie ya msimu uliopita wakati timu hiyo ilipofanya hovyo na kumaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

Baada kutua kuchukua mikoba ya Erik ten Hag akitokea Sporting Lisbon, Amorim aliongoza Man United kushika namba 15 kwenye ligi, huku ikichapwa pia kwenye fainali ya Europa League. Katika kuelekea msimu mpya, Amorim ameomba msaada wa kuongezewa nguvu kwenye benchi.

Kwa mujibu wa gazeti la Ureno, Record, Amorim ametuma maombi binafsi kwa mabosi wakuu wa Man United ili kumleta Acacio Valentim. Valentim, 49, aliyewahi kufanya kazi na Amorim walipokuwa pamoja Braga na sasa anataka wakaungane  Old Trafford.

Mazungumzo yameripotiwa kuendelea ili kuhamia England, hasa baada ya Valentim kuwa huru kufuatia kuachana na klabu hiyo ya Ureno kwenye majira haya ya kiangazi. Ujio wake utakwenda kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la timu hiyo ambalo limekuwa na mabadiliko.

Lililokuwa benchi la ufundi la kocha Erik ten Hag, akiwamo Ruud van Nistelrooy wote waliondoka, huku Rene Hake, Jelle ten Rouwelaar na Pieter Morel nao waliondoka baada ya ujio wa Amorim.

Kocha wa mipira ya adhabu, Andreas Georgson aliwahi alibakizwa, lakini sasa amekabidhiwa majukumu mapya tangu Desemba baada ya Amorim kuthibitisha kwamba msaidizi wake Carlos Fernandes atakuwa na majukumu hayo ya mipira ya adhabu.

Amorim alifanya mabadiliko hayo baada ya mechi ya Arsenal, ambapo Man United iliruhusu mabao kutokana na mipira ya kona, jambo lililoonyesha kocha aliyekuwa akiwajibika na mipira hiyo hakuwa akitimiza wajibu wake sawasawa na hivyo akawekwa kando na mikoba kupewa Fernandes.