Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Chelsea kila mtu anauzwa

Muktasari:

  • Chelsea ipo kwenye majukumu ya kusaka ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu, ambapo usiku wa Jumapili ilikuwa na kibarua cha kumenyana na Benfica huko Marekani.

MIAMI, MAREKANI: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amesema kwenye kikosi chake hicho cha Stamford Bridge hakuna mchezaji yeyote ambaye yupo salama kwa maana ya kupigwa bei katika kipindi hiki dirisha la usajili likiwa wazi.

Chelsea ipo kwenye majukumu ya kusaka ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu, ambapo usiku wa Jumapili ilikuwa na kibarua cha kumenyana na Benfica huko Marekani.

Kikosi cha Chelsea kimefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye siku ya mwisho ya msimu kwenye Ligi Kuu England, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuboresha kikosi chao. Kwa sasa linaloelezwa ni kwamba mabeki wawili, Trevoh Chalobah na Josh Acheampong wanaweza kuondoka licha ya Chalobah, 25, alirudishwa klabuni Januari akitokea Crystal Palace kwa mkop.

Wakati huo, Acheampong, 19 naye yupo kwenye rada za Newcastle na Borussia Dortmund, licha ya beki huyo wa kulia kusaini mkataba mpya mwishoni mwa mwaka jana.

Maresca aliulizwa kuhusu hatima ya wachezaji hao wawili, alisema: “Hadi sasa wachezaji wote waliopo nasi nisingependa kuwapoteza, lakini nimesema mara nyingi ilihali dirisha lipo wazi, basi chochote kinaweza kutokea, hakuna mchezaji ambaye yupo salama, tunaweza kununua na kuuza.”

Kwenye mchezo wa usiku wa Jumamosi wa hatua ya mtoano ya 16 bora, endapo kama kikosi hicho cha Maresca kitakuwa kimepenya, basi kitakuwa na jukumu la kumenyana na moja ya timu mbili za Brazil, Palmeiras au Botafogo, kwenye robo fainali kabla ya uwezekano wa kuwakabili Manchester City kwenye hatua inayoafuatia.