Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Virgil van Dijk amtetea Slot

VAN Pict

Muktasari:

  • Slot alichukua mikoba ya ukocha Anfield mwaka 2024 akimrithi Jurgen Klopp na katika msimu wake wa kwanza aliiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa pointi 84.

LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk amesimama kidete kumlinda kocha anayekosolewa, Arne Slot, akisisitiza licha ya msimu mgumu, Mdachi huyo anastahili kupewa nafasi ya kurejesha mwelekeo.

Slot alichukua mikoba ya ukocha Anfield mwaka 2024 akimrithi Jurgen Klopp na katika msimu wake wa kwanza aliiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa pointi 84.

Hata hivyo, msimu huu haujawa mzuri kwa kikosi cha Slot, ambacho kwa sasa kinashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu. Liverpool imeshinda mechi 11 pekee kati ya 25 za ligi walizocheza msimu huu, wakiwa nyuma kwa pointi 17 dhidi ya vinara Arsenal.

Kufukuzwa kwa Xabi Alonso kutoka Real Madrid mapema mwaka huu kumezidisha tetesi kuhusu mustakabali wa Slot huko Liverpool. Lakini, Van Dijk anaamini kuwa baadhi ya mijadala inayomzunguka kocha huyo wa Kidachi inazidi mipaka ya heshima.

Akizungumza na Sky Sports pamoja na Gary Neville, beki huyo amesema: “Nilisema wiki iliyopita na nimesema hapa tena, ukosoaji, kwa msimu tunaopitia ni wa haki kwa sababu ya namna tulivyokuwa tukicheza wakati mwingine na namna tulivyokuwa tukipoteza mechi mfululizo.

“Hivyo si viwango tulivyojiwekea, hasa baada ya msimu uliopita. Lakini, kuna ukosoaji na kuna kukosa heshima.”

Alipoulizwa kama ukosoaji unaomlenga Slot ni kukosa heshima, Van Dijk alijibu: “Inategemea unavyohisi. Niliulizwa swali hilo wiki iliyopita pia. Je, nadhani kukosa heshima huko kunastahili? Kwa kweli sijui, kwa sababu sisomi kila kitu kila wakati.

“Tuko kwenye mchakato fulani na nahisi inahitaji muda. Sidhani kama Liverpool kwa ninavyofahamu klabu hii, ni klabu inayofanya maamuzi ya pupa; ni klabu inayoamini mchakato. Lakini, najua jinsi dunia inavyofanya kazi na presha ambayo makocha wanakuwa nayo na jinsi wanavyowajibishwa kwa matokeo tunayopata.”