Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu tano zinazothibitisha TFF wako sahihi kuipeleka fainali Pemba

FAINALI Pict


FAINALI ya kumi na moja ya Kombe la Shirikisho la CRDB itafanyika kwenye Uwanja wa Gombani mjini Chakechake, Pemba.


Kama kuna kitu ambacho TFF wamekifanya kwa usahihi na umakini mkubwa, basi ni uamuzi huu.


Sio kila wakati tunawasema vibaya TFF na kuwakosoa, lakini wanapofanya vizuri lazima tuwape maua yao... KONGOLE TFF! Kupitia ukurasa huu nakuletea faida tano kubwa zinazonifanya niwape TFF maua haya.


ALAMA YA TAIFA

Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB ni muendelezo wa Kombe la FA la Uingereza, ambalo ndio mashindano makongwe zaidi ya mpira duniani.

Kwa kuwa Tanzania hatuna chama cha soka (Football Association) bali tuna shirikisho la soka (Football Federation), ndio maana tunaliita Kombe la Shirikisho. Lakini tungekuwa na chama kama zamani wakati wa FAT, tungesema Kombe la FA.

Mashindano ya aina hii yapo dunia nzima na kila nchi huyaita kwa jina linalofanana na mazingira yao kama alama na fahari yao.

Kwa mfano, Hispania wanaliita Kombe la Mfalme, Ureno wanaliita Kombe la Ureno... sawa na Italia. Mashindano haya ni alama ya taifa kupitia mpira na ndio maana fainali yake kwa wenzetu lazima ihudhuriwe na viongozi wakubwa ambao ni alama ya utaifa wao.

Uingereza kwa mfano, lazima mwanafamilia wa ufalme wa Uingereza ahudhurie na ndiye atakayekabidhi Kombe kwa mshindi.

FAIN 01

Haya ni mashindano yanayobeba fahari na utambulisho wa taifa kwenye mpira. Ni sherehe kubwa na yenye kubeba heshima nzito sana.

Kushiriki mashindano haya ni kutafuta nafasi ya kuutambulisha utamaduni na fahari ya watu wa eneo fulani kwenye ngazi ya taifa.

Ukifika fainali unapata nafasi ya kuihadithia nchi stori ya utamaduni na fahari yako. Na hata mahali panapofanyika fainali, yaani uwanja, panapata fursa ya kujitambulisha kitaifa. Kipande chochote cha ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinayo haki hii.


KUUSAMBAZA MPIRA

Mwaka 2017 wakati TFF inaamua kuipeleka Dodoma fainali ya mashindano haya, Rais wake (Jamal Malinzi) alisema lengo ni kuusambaza mpira katika maeneo ambayo mpira hauna mwamko.

Na akasema fainali hii itakuwa ikichezwa kwa mzunguko ili kuhamasisha maendeleo ya mpira wenyewe na miundombinu yake.

2017 - Dodoma

2018 - Arusha

2020 - Sumbawanga (Rukwa)

2021 - Kigoma

2022 - Arusha

2023 - Tanga

2024 - Zanzibar

2025 - Zanzibar

FAIN 02

Huko kote ambako fainali hii imechezwa, ilisaidia kujenga umoja wetu wa kitaifa na kuimarisha miundombinu.

Uamuzi wa kuipeleka fainali maeneo hayo kuliusogeza mpira karibu na mashabiki badala ya kuubakiza Dar es Salaam kama ilivyozoeleka. Pemba inaenda kufaidika kama sehemu nyingine za Tanzania zilivyofaidika na fainali hii katika miaka iliyoandaa.


UCHUMI

Kuipeleka fainali hii maeneo mbalimbali ya nchi kunasaidia kuinua uchumi wa eneo husika. Pemba kwa mfano, kuelekea fainali hii mji huo utapokea wageni wengi sana ambao ujio wao utasaidia kuinua uchumi. Wageni watakaoenda watafanya matumizi kuanzia malazi na malaji.

Matumizi yao yataongeza mzunguko wa pesa na kuisaidia kuinua uchumi. Biashara za wazawa zitaenda kushamiri katika wakati wote wa joto la fainali hii, hadi fainali yenyewe.

FAIN 03

MIUNDOMBINU

Kwa sasa nchi yetu haina viwanja vingi vyenye hadhi ya kupendezesha fainali hii.

Kama sio Gombani basi ingekuwa New Amaan Complex. Hivi ni viwanja pekee nchini vyenye hadhi ya kufanyika fainali ya aina hii bila kuwa na dosari, kuanzia muonekano wa picha za kwenye TV hadi ufundi na mbinu za timu uwanjani.

Sote tuliona mechi ya Simba na Yanga ilipopelekwa Meja Isamuhyo; kuanzia hali ya kiwanja hadi muonekano wa majukwaa kwenye TV.

Mechi kubwa kama hizi zinapaswa kufanyika katika mazingira bora yenye kuvutia kuona na kutumika. Uwanja wa New Amaan Complex umetumika katika fainali mbili zilizopita; si mbaya kwa sasa kutumika uwanja wa Gombani. Na hii ndio namna ya kuwaenzi wawekezaji wa miundombinu ya michezo.

FAIN 04

Wakati England wanacheza uwanja wao wa Wembley, fainali za FA zilifanyika Cardiff, Wales, kwa miaka sita mfululizo, kuanzia 2001 hadi 2006, kwa sababu kwa wakati ule uwanja wa Cardiff ndio ulikidhi zaidi kutokana na kukosekana kwa Wembley.

Kwa sasa uwanja wa Mkapa haupo katika matumizi; New Amaan Complex na Gombani ndio sehemu sahihi zaidi. Viwanja vingine vya mikoani upande wa Bara havina vigezo vya kuchezea fainali hii. Badala ya kukaa na kushangaa, ni busara kuwapigia makofi ya kongole TFF; wamecheza kama Pele.