Ukisikia wameondoka mwisho wa msimu Huu usishtuke!
LONDON, ENGLAND: MASTAA hawa 10 wa Ligi Kuu England ambao wote waliwahi kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu katika klabu zao baadhi hata msimu uliopita tu, lakini sasa wanaweza kuwa njiani kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Bernardo Silva (Man City)
Matumaini ya Pep Guardiola ya Silva abaki milele yameongeza kwa kasi uvumi wa kuondoka kwake majira ya kiangazi, hasa mkataba wake unapokaribia kumalizika. Inasemekana anaitaka Barcelona zaidi ya yote.
Kauli ya Guardiola kwamba hulala vizuri zaidi akimweka Silva kwenye kikosi na hilo ni “muhimu kwa afya yangu” inaashiria huenda ni bora kwa pande zote mbili wakiachana, kabla Silva hajagundua madhabahu iliyojengwa kwa heshima yake kwenye chumba cha pili cha kulala cha kocha wake, au Guardiola kabla hajachora tattoo ya sura ya Silva mgongoni.
Martin Odegaard (Arsenal)
Mchawi mpya wa kulaumiwa Arsenal na ni vigumu kupinga chaguo hilo kwa mashabiki wa The Gunners. Hakuridhisha aliporejea kutoka majeraha msimu uliopita, lakini msimu huu isipokuwa maonyesho machache mazuri Ødegaard anaonekana kupoteza karibu kabisa ubunifu, maono ya pasi na uwezo wa kuzitekeleza.
Kupiga pasi za mita 10 kwenda miguuni mwa Bukayo Saka hakutoshi kwa mchezaji anayetarajiwa kuongoza ubunifu wa timu inayowania ubingwa. Kuendelea kwake kuanza kikosi ni jambo linalokera sana kwa wale wanaotaka akae benchi huku Eberechi Eze akitazama kutoka pembeni.
Virgil van Dijk (Liverpool)
Wachezaji kulaumu upepo kama alivyofanya Van Dijk baada ya kosa lake kusababisha bao la kwanza la Bournemouth, Jumamosi kutawafanya wale wanywaji wa bia wa kilo 120 kwenye pabu kucheka kwa sauti wakisema, “analipwa pesa ngapi tena?”
Hata hivyo, upepo ni kitu halisi na kwa kweli hufanya kuondoa mpira juu ya bega lako kuwa kugumu zaidi.
Kile ambacho Van Dijk hakukieleza ni kwa nini aliongeza kosa lake kwa kushindwa kabisa kujaribu kuzuia krosi ya Alex Jimenez na kwa nini anasisitiza kumtazama mtu mwingine wa kulaumiwa ilhali kosa lilikuwa lake peke yake.
Hii haikuwa mara ya kwanza msimu huu kuonyesha uzembe wa akili na mwili kutoka kwa mchezaji ambaye inazidi kuwa vigumu kumwona kama nguzo ya timu ya ubingwa wa baadaye. Hivyo, chochote kinaweza kutokea mwisho wa msimu.
Mohamed Salah (Liverpool)
Hakuwa kwenye ubora wake kabisa katika kipigo dhidi ya Bournemouth, isipokuwa mipigo michache ya kuchekesha iliyokosa mwelekeo, jambo linaloimarisha nadharia kuwa sio tu amepunguza mwendo baada ya kupewa mkataba mnono mpya, bali amezima kabisa injini na kutupa funguo nje ya gari.
Kinachodhaniwa ni huenda sababu zinazowezekana zaidi ni Salah sasa ni mkubwa kwa mwaka mmoja na hivyo si mkali kama awali, hajazoeana na wachezaji wapya kikosini, au kwa uwezekano mkubwa mchanganyiko wa mambo hayo.
Chochote sababu, hakuna nafasi katika timu kwa mchezaji anayechangia kidogo kiasi hicho, hasa baada ya kusababisha mvutano mkubwa baada ya kukaa benchi mechi mbili na kutibuana na kocha Arne Slot.
Cole Palmer (Chelsea)
Palmer anadaiwa kuwa “mwenye furaha sana” Chelsea licha ya ripoti za kukumbuka maisha ya nyumbani kwao jijini Manchester na kuibuka kwa uvumi wa kuhusishwa na Manchester United, anasisitiza Liam Rosenior baada ya “mazungumzo mengi” na mchezaji huyo wa England.
Unajua yale mazungumzo ambayo msemaji hakati macho hata kidogo kana kwamba anaamini ni siri ya mawasiliano bora, lakini kwa kweli humfanya anayesikiliza ajisikie vibaya kiasi cha kukubali chochote kama kusema anataka kubaki klabuni ili tu kumaliza mazungumzo hayo haraka, ambayo inadhaniwa Rosenior anataka kutuliza presha ya kumhusu Palmer, lakini katika kuelekea mwisho wa msimu, chochote kinaweza kutokea.
Luke Shaw (Man United)
Shaw ameanza mechi zote 23 za Man United za Ligi Kuu msimu huu, huku kiwango chake cha hivi karibuni kikionyesha kwamba mchezaji huyo wa miaka 30 yuko kwenye kipindi kingine cha kujikomboa katika maisha yake ya miaka 11 na nusu Old Trafford yaliyojaa kupanda na kushuka.
Kwa kuzingatia hali hiyo na mkataba wake unaoisha 2027, kumuuza Shaw wakati kiwango chake kiko juu kuna mantiki kubwa.
Na kwenye hilo, ndiyo maana kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kitu wakati wa msimu huu utakapofika mwisho na dirisha la usajili wa majira ya kiangazi utakapofunguliwa.
Emiliano Martínez (Aston Villa)
Alijaribu kwa makusudi kushinikiza uhamisho wa kwenda Manchester United dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini Aston Villa waligoma kumwaachia na sasa wamelenga kupiga pesa nyingi, wakibainisha bei ya kipa huyo anayouzwa kuwa ni Pauni 40 milioni.
Martínez ameokoa 76.1% ya mashuti aliyokabiliwa nayo msimu huu kiwango cha juu zaidi kwenye ligi nzima, lakini hakuna mchezaji aliyehusika na makosa mengi yaliyopelekea mabao kuliko makosa yake matatu.
Bruno Fernandes (Man United)
Fernandes yuko katika nafasi ya kuiweka Man United pabaya kwenye majira ya joto yajayo na watalazimika ama kumpa mkataba mpya mnono sana kabla hajafikisha miaka 32 Septemba, au wakabiliane na kazi ngumu ya kutafuta mrithi wake.
Kile wasichopaswa kabisa kufanya ni kumruhusu amalize mkataba wake na kuondoka bure mwaka 2027, ilhali kuna klabu nyingi zilizo tayari kulipa pesa nyingi kwa ajili ya kunasa saini yake.
Kutokana na hilo, lolote linaweza kutokea kwa Fernandes juu ya mustakabali wa maisha yake baada ya msimu huu kumalizika.
Micky van de Ven (Tottenham)
Kauli ya Thomas Frank kwamba “Micky ni mchezaji wa Tottenham sasa na kwa siku zijazo” ni sawa na muuzaji wa nyumba kusisitiza sakafu ya marumaru isiguswe kabla ya kukabidhi funguo.
Kuweka bei ya Pauni 100 milioni kwa Van de Ven huenda kutaongeza tu dhamira yake ya kuondoka klabuni haraka iwezekanavyo, kwani ni wazi Tottenham si mahali sahihi kwa beki wa kati wa thamani ya tarakimu tisa.
Kuna mambo mengi, lakini upo uwezekano pia wa beki huyo akaachana na Spurs mwisho wa msimu bila ya hataka kulipwa nusu ya pesa hiyo iliyotajwa.
Ollie Watkins (Aston Villa)
Amerudi kwenye kiwango kizuri hivi karibuni, akifunga mabao saba katika mechi zake 10 za mwisho za Ligi Kuu England, baada ya mwanzo mbaya wa msimu na alifunga bao moja tu katika mechi 13.
Hata hivyo, karibu kila dirisha la usajili hupita akiwa anahusishwa na kuondoka. Nafasi ya kujiunga na klabu kubwa zaidi huenda ilishapita, lakini Aston Villa inapanga kuleta ushindani mpya kwenye nafasi yake mwezi huu na kutokana na hisia ya muda mrefu kuwa anaamini nyasi ni kijani zaidi kwingineko, Watkins anaweza kushinikiza zaidi uhamisho.