Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vichapo vya msuta Wilder kustaafu ngumi

Muktasari:

  • Hata hivyo, bondia huyo ameondoka Saudia Arabia lilikopigwa pambano hilo bila kuweka wazi juu ya kauli yake hiyo kama ataitimiza au ataendelea kupanda ulingoni.

KABLA ya kupanda ulingoni kukipiga dhidi ya bondia Zhilei Zhang, Alfajiri ya Jumapili iliyopita, bondia Deontay Wilder alisisitiza kwa tambo nyingi hatapigwa na Zhang na ikitokea akapoteana, ataachana na ngumi kabisa kenye usiku huo uliokuwa na mapambano mengine makali.

Hata hivyo, bondia huyo ameondoka Saudia Arabia lilikopigwa pambano hilo bila kuweka wazi juu ya kauli yake hiyo kama ataitimiza au ataendelea kupanda ulingoni.

Wilder alipoingia ulingoni, alikuwa na imani kubwa sana ya kushinda pambano hilo dhidi ya Mchina huyo ambaye naye pia alichapwa na bondia Joseph Parker.

Katika pambano hilo, lilianza na mambo yalikuwa tofauti kwa Wilder kutokana na makonde mazito mfululizo aliyoyapata kutoka kwa Zhang.

Hata hivyo, raundi ya tano tu, mambo yakawa sio mambo kwa Wilder na  alitandikwa ‘vibaya’ na kuanguka chini kama mzigo, kiasi cha mwamuzi kumaliza pambano na hata baada ya Wilder kuinuka, hakuweza kumshawishi mwamuzi kumruhusu aendelee na pambano hilo.