Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Modric Madrid yamnyatia Mac Allister

Muktasari:

  • Licha ya nia ya kutaka kumsajili Mac Allister, taarifa zinaeleza kwamba dili hilo lina asilimia ndogo za kukamilika  kwani Liverpool haina mpango wa kumuuza.

REAL Madrid ina mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya Argentina, Alexis Mac Allister ili akawe mrithi wa kiungo raia wa Croatia, Luka Modric, 39, ambaye ametangaza kuwa ataondoka mwisho wa msimu huu.

Licha ya nia ya kutaka kumsajili Mac Allister, taarifa zinaeleza kwamba dili hilo lina asilimia ndogo za kukamilika  kwani Liverpool haina mpango wa kumuuza.

Mabosi wa Liverpool hawataki Mac Allister aondoke kwa sababu atakuwa ni mchezaji wa pili tegemeo katika kikosi kufanya hivyo kwenye dirisha lijalo baada ya Trent Alexander Arnold ambaye atajiunga na Real Madrid baada ya mkataba wake kumalizika.

Mkataba wa sasa wa nyota huyo unatarajiwa kumalizika 2028 na msimu huu amecheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao saba.


Alejandro Garnacho

WINGA wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Garnacho mwenye umri wa miaka 20 anaonekana kuwa karibu zaidi kuondoka kwenye kikosi hicho katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa kwamba Garnacho ambaye anawindwa sana na Atletico Madrid haoni nafasi yake katika kikosi cha Man United chini ya Ruben Amorim.


Florian Wirtz

KIUNGO wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz, 22, anaripotiwa kuwa angependelea zaidi kujiunga na Liverpool badala ya Bayern Munich katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Wirtz ambaye awali alitajwa  kutakiwa na Man City kabla ya dili halijaota mbaya anataka kucheza nje ya Ujerumani hususan Ligi Kuu England ambako ni ndoto yake ya muda mrefu.


Kaoru Mitoma

BAYERN Munich inaamini kuwa winga wa Brighton na timu ya taifa ya Japan, Kaoru Mitoma, 28, ataisaidia sana katika eneo  la kiungo ikiwa itaipata saini yake katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mitoma ambaye mwaka jana alihusishwa na timu kadhaa za Saudi Arabia zilizokuwa tayari kutoa ada ya uhamisho ya Pauni 90 milioni, lakini alikataa kujiunga nazo. Mkataba wake unamalizika 2027.


Liam Delap

EVERTON imefanya mazungumzo na Ipswich kuhusu mshambuliaji wa timu hiyo na England, Liam Delap, 22, ili kuona uwezekano wa kuipata saini yake katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mabosi wa Everton wamedhamiria kuboresha eneo la ushambuliaji na mbali ya Delap pia wanaitaka saini ya winga wa Liverpool na Scotland, Ben Doak mwenye umri wa miaka 19.


Benjamin Sesko

MAZUNGUMZO kati ya mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal, Andrea Berta na wawakilishi wa RB Leipzig yanadaiwa kufikia patamu na kuna uwezekano mkubwa Washika Mitutu hao wakakamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Slovenia, Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 21. Msimu huu Sesko amecheza mechi 45 za michuano yote na kufunga mabao 21.


Matheus Cunha

MSHAMBULIAJI wa Wolves na timu ya taifa ya Brazil, Matheus Cunha, 25, ana mpango wa kutaka kujiunga na Manchester United katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya kimataifa msimu ujao. Cunha ambaye anahitajika na vigogo wengi Ulaya mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029.


Matheus Fernandes

AASTON Villa, West Ham United na Leeds United zote zinamfuatilia kwa karibu kiungo wa Southampton na timu ya taifa ya Ureno chini ya miaka 21, Matheus Fernandes, 20 ili kumsajili dirisha lijalo. Fernandes ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029, msimu huu amecheza mechi 43 za michuano yote na kufunga mabao matatu.