Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usajili unaobamba NBA, Lakers pagumu

Muktasari:

  • Dirisha kubwa la usajili linaloendelea ndilo kwa kiasi kikubwa huwa na idadi kubwa ya wachezaji kuhama au kuhamishwa kwa makubaliano ya timu zaidi ya moja kuanzia  mbili, tatu hadi nne na kuendelea kulingana na makubaliano ya timu husika.

DIRISHA la usajili wa wachezaji kutoka timu moja kwenda nyingine katika Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), unaendelea ambapo tayari kuna majina makubwa yameshahamishia ustaa katika timu mpya huku wengine wakizua gumzo kwenda upande ambao haukutarajiwa na kutokwenda pale ilipofikiriwa na wengi.

Dirisha kubwa la usajili linaloendelea ndilo kwa kiasi kikubwa huwa na idadi kubwa ya wachezaji kuhama au kuhamishwa kwa makubaliano ya timu zaidi ya moja kuanzia  mbili, tatu hadi nne na kuendelea kulingana na makubaliano ya timu husika.

Uhamisho huo hubebwa kwa ukubwa na chaguo la wachezaji wa kwenye drafti ya kila msimu ambao hutangulia kabla ya kufuata usajili wa wachezaji waliopo kwenye ligi.

Kutokana na ukubwa wa dirisha hili, hadi sasa upo usajili uliofanyika na kushangaza licha ya kuwa kawaida kutokea kwenye dirisha hili ila ni jinsi ambavyo mambo yanaenda vyema kwa baadhi ya timu na wachezaji.

Zipo baadhi ya timu ikiwemo Los Angeles Lakers ambayo imewekewa matarajio makubwa, lakini ndio imefeli hadi sasa kunasa wachezaji iliowatarajia.


KLAY THOMPSON KWENDA DALLAS

Hilo ndilo jina kubwa ambalo limeshtua wengi kwa kuondoka kwenye timu aliyoanzia kucheza NBA, Golden State Warriors, na kujiunga na Dallas Mavericks bila kutarajiwa na wengi ambao waliamini ataondoka, lakini sio kujiunga na Dallas badala yake iliaminika atajiunga na Los Angeles Lakers.

Siyo tu mashabiki na wafuatiliaji wa ligi hiyo ambao walishtushwa na kitendo cha Klay kuichagua Dallas badala ya Lakers, bali hata baba yake mzazi, Mychal Thompson hakuamini kilichotokea kwa mwanaye kujiunga na Mavericks. Mzazi huyo alijua na alishasema wazi kuwa atafurahi mtoto wake kujiunga katika timu moja na LeBron James pale Los Angeles wakati huu wakielekea ukingoni mwa ubora wao.

Klay kujiunga kwake Dallas kunamaanisha anaongeza nguvu mpya kwa mastaa Luka Doncic na Kyrie Irving ambao kwa pamoja na nyota wengine walifanikiwa kucheza fainali ya NBA msimu ulioisha.

Dallas walifungwa na Boston Celtics kwa matokeo ya 4-1 za mechi tano pekee isivyotarajiwa na wengi, lakini uwepo wa Klay na kama atarudisha makali yake, ni silaha mpya kwao.


LEBRON KUBAKI LAKERS

Kabla ya uamuzi wa LeBron James kuongeza mkataba mpya kubaki Los Angeles Lakers, lilitangulia dili la mwanaye, Bronny James ambaye alichaguliwa na timu hiyo kama chaguo la 55 katika drafti na amepewa miaka minne kuitumikia timu hiyo.

Taarifa zinamtaja kupelekwa kwanza timu ya chini (G League) kabla ya kuiva na kuanza kucheza timu kubwa pamoja na baba yake.

Kubaki kwa LeBron, awali kulikuwa na matarajio ya ujio wa majina makubwa ndani ya timu hiyo kiasi cha kuwa tayari kupunguza mshahara wake ili tu kufanikisha nyota wengine bora wajiunge na kuanzia Klay ambaye hata hivyo ameichagua Dallas.

Vilevile kuna DeMar DeRozan kutoka Chicago Bulls ambaye hata hivyo bado hakuna uhakika wa kujiunga na timu hiyo na mkali wa pointi tatu, Buddy Hield aliyesema timu hiyo haina uhakika wa ubingwa kama Warriors.


PG13 NA UTATU MPYA 76ERS

Dili lingine kubwa ambalo halikutarajiwa kutokea ni kwa staa Paul George ‘PG13’ kuitema Los Angeles Clippers na kujiunga na Philadelphia 76ers ambapo anakwenda kutengeneza utatu mpya ‘trio’ mkali pamoja na mastaa Joel Embiid na Tyrese Maxey katika jitihada za kuifanya timu hiyo kuwa na makali zaidi baada ya awali kushindwa alipojiunga nayo James Harden.

PG13 alishangaza kuondoka Clippers kwa sasabu alikaririwa akisema kwamba atastaafia kwenye timu hiyo ya Magharibi, lakini ameshindwa kulinda ahadi yake na kwenda ukanda wa Mashariki kujiunga na Sixers msimu ujao.


HIELD, CURRY BALAA

Baada ya Golden State Warriors kumuachia Klay kuondoka na kujiunga na Dallas, timu hiyo imeziba pengo kwa kumnasa supastaa Buddy Hield kutoka Philadelphia 76ers iliyomsajili Paul George.

Kutokana na usajili huo hivi sasa Hield anaungana na mkali mwenzake wa mitupo ya pointi tatu kwenye ligi, Stephen Curry.

Kwa msimu wa tano mtawalia Hield amekuwa kwenye vita kali ya kurusha mitupo mingi zaidi ya pointi tatu dhidi ya Steph Curry tangu akiwa Indiana Pacers na sasa anakwenda kuungana na mpinzani wake mkubwa kwenye pointi tatu, Chef Curry