Ufahamu uwanja uliotelekezwa kwenye msitu mnene Ukraine

LONDON, ENGLAND. UWANJA wa zamani wa Avanhard wa mpira ambao ulikuwa ukiingiza mashabiki 5,000, uliachwa kutumika baada ya maafa ya Chernobyl 1986 kufuatia utafiti uliofanywa hivi karibuni na Gazeti la The Sun.

Avanhard ulikuwa uwanja wa nyumbani wa Soviet FC Stroitel Pripyat huko Ukraine ambayo ilishiriki Ligi Daraja Nne iliyoanzishwa 1970. Timu hiyo ilishinda mashindano ya soka ya Mkoa wa Kyiv miaka mitatu mfululizo kuanzia 1981 hadi 1983 kwa mujibu wa historia kabla ya kupata umaarufu. Hata hivyo timu hiyo haipo tena.

Lakini kutokana na tukio la kihistoria la mlipuko wa nyuklia ambao uliikumba miji yote iliyopo Kaskazini mwa Ukraine - siku ambayo FC Stroitel Pripyat ilikuwa ikijiandaa na mchezo wa nusu fainali ya dhidi ya FC Borodyanka.

Kutokana na mlipuko wa nguvu wa nyuklia ulitokea karibu na Miji ya Pripyat na Chernobyl umbali wa kilomita 100 Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Ukraine wa Kyiv.

Asili ya mlipuko huo ulitokea na kuharibu maeneo hayo kwa muda dakika 11 kutoka Uwanja wa Avanhard. Watu walilazimika kuhama umbali wa maili 18 kutoka uwanja huo. Hiyo ilitokana na mlipuko wa nyuklia ambao ulileta madhara makubwa.
FC Stroitel Pripyat haikucheza mechi kwa msimu uliobakia kabla ya kubadilisha jina la timu na kuitwa FC Stroitel Slavutych mwaka uliofuata na hatimaye kufutwa.

Hata hivyo, licha ya hali mbaya ya hewa iliyoachwa baada ya maafa hayo, sehemu za uwanja wa klabu hiyo bado zimefunikwa na msitu mnene mpaka leo na kuwa kivutio kwa watu wanaopita katika maeneo hayo baada ya kupotezewa kwa muda mrefu hata hivyo, hakuna dalili ya makazi ya watu wanaoishi katika eneo hilo.

Ukiangalia eneo hilo ni ngumu kupata ardhi kutokana na kijani kibichi kilichotanda katika uwanja huo. Lakini picha kadhaa zilizopigwa na watafiti hivi karibuni zinaonesha sehemu za kukalia mashabiki kwa mbali hata hivyo mbao zake zimeharibika vibaya.

Utafiti ulioendelea ni kwamba sehemu kubwa uwanja huo imefunikwa na miti pamoja na majukwaa ya kukalia mashabiki. Lakini milango ya kuingilia mashabiki imeonekana vizuri na haikuzungukwa na msitu mnene.
Kutokana na uwanja huo kutotumika kwa muda mrefu taarifa zimeripoti hakuna uwezekano wa kuukarabi upya siku za usoni.