Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United imejipanga, yatenga Pauni 125 milioni

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Man United inahitaji fowadi mpya ili kuifanya timu hiyo kuwa tishio zaidi na hilo linafanyiwa kazi na kocha Ruben Amorim ili kuhakikisha anaunda timu itakayokuwa na uwezo wa kufunga mabao kwenye kila mechi.

MANCHESTER, ENGLAND: NUSU fainali ya Europa League si umeona? Basi Manchester United imejipanga kwa mazuri zaidi kwenye kikosi hicho baada ya kutenga mkwanja wa Pauni 125 milioni kunasa huduma ya wakali wawili kwenye Ligi Kuu England, Bryan Mbeumo na Matheus Cunha.

Man United inahitaji fowadi mpya ili kuifanya timu hiyo kuwa tishio zaidi na hilo linafanyiwa kazi na kocha Ruben Amorim ili kuhakikisha anaunda timu itakayokuwa na uwezo wa kufunga mabao kwenye kila mechi.

Miamba hiyo ya Old Trafford ipo tayari kuwauza Marcus Rashford na Antony mwishoni mwa msimu huu baada ya wote kuwatoa kwa mkopo kwenye dirisha la Januari, wakati huko Rasmus Hojlund na Alejandro Garnacho wakisubiri kuona kama kutakuwa na ofa za maana zitakazowekwa mezani ili wapigwe bei.

Hata hivyo, Garnacho alisema anataka kubaki Man United kwa miaka mingi zaidi, huku Hojlund akidaiwa kwamba anaweza kutumika kwenye dili la kubadishana wachezaji na klabu ya Liverpool. Hivi karibuni iliripotiwa kwamba kwenye kikosi cha Man United kwa sasa ni wachezaji wanne tu wenye uhakika wa kubaki, ambao ni Bruno Fernandes, Harry Maguire, Amad Diallo na Patrick Dorgu, lakini waliobaki wote watawekwa sokoni kusubiri ofa ya maana iletwe.

Hilo linakuja baada ya mabosi wa Man United kutaka huduma za wachezaji Mbeumo na Cunha, ambao wanaamini watakwenda kukibadili kikosi hicho kinachonolewa na Mreno Amorim. Fowadi wa Wolves, Cunha, 25, kwa wiki za karibuni amekuwa akihusishwa sana na Man United na miamba hiyo ya Old Trafford inajiandaa kulipa Pauni 65 milioni kunasa huduma yake kama kinavyobainisha kipengele kwenye mkataba wa mkali huyo wa Molineux.

Na sasa ripoti nyingine inafichua kwamba Man United ipo kwenye mbio za kumfukuzia Mbeumo, ambaye anatajwa kuwa na thamani ya Pauni 60 milioni. Winga huyo wa Brentford amekuwa akisakwa na timu nyingi ikiwamo Arsenal, Liverpool na Newcastle United baada ya kufunga mabao 18 na kuasisti mara sita kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Man United usiku wa Alhamisi ilikuwa na kibarua cha kurudiana na Athletic Bilbao kwenye nusu fainali ya Europa League uwanjani Old Trafford, huku miamba hiyo ya England iliingia ikiwa mbele kwa mabao 3-0 ya mechi ya kwanza.