Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tumeonewa… Arteta awaka kunyimwa penalti ya wazi

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arsenal ilishindwa kutumia fursa ya kuongeza pengo la alama hadi pointi tisa dhidi ya wapinzani wao wa ubingwa, Manchester City, kileleni mwa Ligi Kuu England, baada ya kuonyesha kiwango cha chini dhidi ya Forest na kutoka sare hiyo isiyo na mabao.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema anaamini timu hiyo ilipaswa kupewa 'penalti ya wazi kabisa' katika mechi ya juzi usiku ya Ligi Kuu England dhidi ya Nottingham Forest iliyomalizika kwa suluhu.

Arsenal ilishindwa kutumia fursa ya kuongeza pengo la alama hadi pointi tisa dhidi ya wapinzani wao wa ubingwa, Manchester City, kileleni mwa Ligi Kuu England, baada ya kuonyesha kiwango cha chini dhidi ya Forest na kutoka sare hiyo isiyo na mabao.

VAR ilipuuza maombi ya benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa Arsenal waliokuwa wanasisistiza staa wa Forest, Ola Aina alikuwa ameshika katika boksi.

Hata hivyo, Arsenal hawakuonekana kuwa na makali makubwa mbele ya lango katika mechi hiyo, lakini Arteta anaamini walistahili kupewa nafasi ya dhahabu ya kuongoza kwa penalti baada ya mpira kugonga mkono wa Ola Aina ndani ya eneo la hatari.

Aina alionekana kuugusa mpira kwa mkono wa kulia alipokuwa akijaribu kuuzuia usitoke nje mwishoni mwa kipindi cha pili, lakini VAR iliamua tukio hilo halikuwa penalti, ikieleza kuwa mkono wa beki huyo ulikuwa katika 'nafasi ya kawaida'.

Hilo halikumzuia Arteta kuweka wazi kabisa msimamo wake baada ya mechi kumalizika na akizungumza na BBC amesema: "Tumetengeneza nafasi nne kubwa, kubwa sana, pamoja na penalti ya wazi, lakini hatukuweza kushinda mechi. Nimeangalia marudio ya tukio na nadhani yule mchezaji alikuwa akifanya jaribio la wazi la kuondoa mpira akiwa ndani ya eneo la boksi na naamini ilikuwa ni penalti ya wazi kabisa, hivyo sielewi kwa nini hatukupewa."

ART 02

Kocha wa Forest, Sean Dyche alikuwa na mtazamo tofauti kabisa na akizungumza na TNT Sports, amesema: "Ikiwa mnasema ile ilikuwa ni penalti ni bora tuachane kabisa na mpira wa miguu, kwa sababu ni wazi kabisa ile haikuwa penalti na kila kitu kilikuwa kinajionyesha."

Akizungumza na SunSport, aliyekuwa refa wa Ligi Kuu, Mark Halsey, amesema:

"Kulikuwa na tukio lililoonyesha mpira kugonga mkono wa Ola Aina. Mimi binafsi nasema ni kweli mpira uligonga mkono wake, lakini kwa maoni yangu, mikono yake ilikuwa katika nafasi ya kawaida na halisi. Mikono yake ilikuwa juu ikishuka wakati mpira nao unashuka. Ndiyo, uligonga mkono wake, lakini haikuwa kwa makusudi. Hivyo kwa maoni yangu, Michael Oliver na VAR walifanya uamuzi sahihi kabisa. Sioni kama ilikuwa penalti.”

Arteta alikiri pia timu yake inapaswa kutumia vyema zaidi nafasi wanazotengeneza, badala ya kutegemea maamuzi ya waamuzi.

Aliongeza: “Tungefanya vizuri zaidi, pia hili linatokea kwa kila timu kwenye ligi. Tunapaswa kuboresha kiwango chetu, hasa tunapotengeneza nafasi nne kubwa, lazima uzifunge.

“Lazima utengeneze ile hali ya kutumia vizuri nafasi hizo. Lakini mwisho wa yote niseme wanastahili pongezi, pia kwa sababu walicheza vizuri."

ART 03
ART 03

"Mwishoni tulijaribu kutafuta bao. Sidhani kama walipata hata shuti moja, lakini hatukuweza kuwafungua na hiyo ni kawaida katika mchezo huu."

Gabriel Martinelli, aliyefunga hat-trick katika Kombe la FA mwishoni mwa wiki iliyopita, alitoka kuwa shujaa hadi kuwa mwangushaji timu baada ya kukosa bao la wazi kipindi cha kwanza.

Hata hivyo, Arsenal iliongeza uongozi wao kileleni mwa msimamo wa ligi hadi kufikia pointi saba baada ya Manchester City kufungwa mabao 2-0 na Manchester United katika dabi ya Manchester.