Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zubimendi azidi kumvuruga Arteta

ZUBIMENDI Pict

Muktasari:

  • Nyota wa Hispania, Zubimendi amekuwa gumzo tangu ajiunge na Arsenal akitokea Real Sociedad msimu uliopita wa kiangazi kwa ada ya Pauni 51 milioni.

LONDON, ENGLAND: MIKEL Arteta mara chache hukosa maneno, lakini anaishiwa na la kusema kuhusu Martin Zubimendi.

Nyota wa Hispania, Zubimendi amekuwa gumzo tangu ajiunge na Arsenal akitokea Real Sociedad msimu uliopita wa kiangazi kwa ada ya Pauni 51 milioni.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 alibainishwa na timu ya usajili ya Arsenal kwa sababu waliamini angeweza kuwa moyo wa mchezo wa kikosi cha Arteta.

Hata hivyo, kiwango cha Zubimendi kimeendelea kukua na sasa amegeuka kuwa silaha hatari pia katika ushambuliaji.

ZUBI 01

Zubimendi alifunga bao la ushindi dhidi ya Chelsea, Jumatano usiku katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi. Mhispaniola huyo sasa amefunga mabao manne msimu huu, huku pia akichangia asisti tatu.

Tayari huu ni msimu wake bora zaidi kwa upande wa mchango wa ushambuliaji na bado zimesalia zaidi ya miezi minne kabla ya msimu kumalizika.

Arteta amesema: “Tulipozungumzia Zubi, tuliulizana kama anaweza kufanya nini kingine? Na ukweli, anaweza kufanya chochote anachotaka. Ni kidogo kama sifa za Declan Rice. Tunahitaji tu kuendelea kufungua hilo katika mfumo wake, katika akili yake, kwa sababu yeye ni mzuri sana katika kuchukua nafasi tofauti, kubeba mpira, kupiga chenga, kushinda mapambano. Na ana kipaji kwamba anapofika hatua ya mwisho na ndani ya boksi, huwa mtulivu sana. Anaona picha kwa uwazi mkubwa.â€

Kufunguka kwa uwezo wa Zubimendi katika ushambuliaji ni habari njema kwa Arsenal, ambayo bado haina mshambuliaji wa kuaminika wa kufunga mabao mengi.

Viktor Gyokeres alifunga katika ushindi wa Jumatano dhidi ya Chelsea, lakini ana mabao manane pekee msimu huu.

ZUBI 03

Mshambuliaji huyo wa Sweden hajatimiza matarajio ya kuwa mashine ya mabao kama wengi walivyotarajia wakati Arsenal walipolipa ada ya awali ya Pauni 54.8 milioni kutoka Sporting Lisbon kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Hali hiyo imesababisha Arsenal kusambaza mabao kwa wachezaji wengi na Zubimendi ni mfano bora wa hilo. Kikosi cha Arteta kimepata wafungaji 16 tofauti msimu huu na kimefaidika na mabao ya kujifunga. Gabriel Martinelli akiwa kinara akiwa na mabao tisa.

Hali hiyo ni tofauti kabisa na wapinzani wao wakubwa kwenye mbio za ubingwa, Manchester City, ambao wanaongozwa na Erling Haaland mwenye mabao 20 kwenye Ligi Kuu England. Wafungaji bora wa Arsenal kwenye Ligi Kuu ni Leandro Trossard na Gyokeres, kila mmoja akiwa na mabao matano.