Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuchel avurugwa na kanuni...

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Chelsea, Thomas Tuchel ameonekana kushangazwa na kitendo cha bao la mshambuliaji wake, Timo Werner kukataliwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambao iliwabidi kufanya kazi ya ziada ili kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya watakatifu,  Southampton.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Stamford Bridge, Tuchel amesema, "Kabla ya msimu kuanza tulifanya mazungumzo. Kila mtu aliniambia tunarejea kwenye ligi ya soka la England (EPL) na hakutakuwa na filimbi za faulo za kawaida na itategemea mchezo unaendaje."

"Kisha tupo hapa katikati ya jiji la London, mvua inanyesha, ni kama dakika ya 40 ya mchezo, kwenye mechi ngumu na sio kwenye tukio la moja kwa moja likafungwa goli, kulikuwa na nafasi, kisha nafasi nyengine, ikapigwa krosi, kisha goli likafungwa kisha tunarudi tena."

"Tukio lile halikuwa na madhara makubwa kwenye kufungwa kwa goli. Kwahiyo mpaka sasa nina uelewa sifuri wa kwanini goli lilikataliwa," amesema.

Upande wake Werner ambaye amefikisha jumla ya mabao  16 yaliyokataliwa amesema, " Sikutegemea kama ingekuwa vile. Lakini inavunja moyo, unafunga, kisha unashangilia na mashabiki kisha unaenda kati na unaambiwa goli lako limekataliwa."

"Mara 16 ndani ya mwaka mmoja? Ni jambo gumu lakini naendelea kusonga mbele."

Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kwenye mchezo huo kupitia kwa Trevoh Chalobah lakini Southampton wakasawazisha kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Ward-Prowse J. ambaye hata hivyo alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 77 baada ya mchezea faulo mbaya Jorginho

Kitendo cha Southampton kuwa pungufu ilikuwa faida kwa Chelsea kwani walitumia mwanya huo kusukuma mashambulizi mfululizo na mwishowe kupata mabao mengine mawili ambayo yalifungwa na Werner pamoja na beki, Chilwell.