Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tomiyasu achana mkataba Arsenal

TUMIYASU Pict

Muktasari:

  • Tomiyasu, 26, amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa, ambao ulikuwa na kipengele cha kuongeza miezi 12. Na ripoti sasa zinafichua beki huyo wa pembeni alifikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa Arsenal, Takehiro Tomiyasu anaachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya kusitisha mkataba wake.

Tomiyasu, 26, amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa, ambao ulikuwa na kipengele cha kuongeza miezi 12. Na ripoti sasa zinafichua beki huyo wa pembeni alifikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake.

Jambo hilo linahitimisha maisha ya Mjapani huyo ambaye amekuwa akisumbuliwa sana na majeraha katika miaka yake minne kwenye kikosi cha Emirates.

Tangu usajili wake wa Pauni 20 milioni aliponaswa na Arsenal kutokea Bologna mwaka 2021, Tomiyasu amekumbwa na nyakati ngumu za kuumia mara nane tofauti.

Tatizo lake la hivi karibuni lililomgharimu beki huyo wa kulia ni wakati alipoumia goti na kumfanya acheze kwa dakika sita tu msimu uliopita. Beki huyo alilazimika kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitano baada ya kufanyiwa upasuaji, Februari mwaka huu.

Mjapani huyo alikosa mwanzo wa msimu uliopita kutokana na tatizo hilo la goti, ambalo lilihitaji kufanyiwa upasuaji 2023.

Shabiki wa Arsenal aliandika kwenye Twitter: "Ah, nilimpenda mchezaji. Imekuwaje tena..."

Mwingine alisema: "Huzuni kubwa. Nikumtakia tu kila la heri huko aendako.

Shabiki wa tatu aliandika: "Namtakia kila la heri. Majeraha yamemharibia mchezaji mahiri sana."

Mwingine alisema: "Tutamkumbuka sana. Kila la heri Tomi."

Tomiyasu alicheza mechi 84 kwenye kikosi hicho cha Arsenal kwa kipindi cha miaka minne.