Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TETESI USAJILI ULAYA: Barca kupambana Cancelo, Felix wabaki Nou Camp

Muktasari:

  • Cancelo na Felix walicheza Barcelona kwa mkopo wakitokea Manchester City na Atletico Madrid mtawalia na baada ya viwango vyao bora kwa msimu wa 2023-24, uongozi wa miamba hiyo ya Nou Camp sasa unafikiria kubaki nao kwenye timu.

RAIS wa Barcelona, Joan Laporta amesema klabu hiyo kwa sasa ipo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kuwabakiza kikosini mastaa, Joao Cancelo na Joao Felix kwa ajili ya msimu wa 2024-25.

Cancelo na Felix walicheza Barcelona kwa mkopo wakitokea Manchester City na Atletico Madrid mtawalia na baada ya viwango vyao bora kwa msimu wa 2023-24, uongozi wa miamba hiyo ya Nou Camp sasa unafikiria kubaki nao kwenye timu.

Wachezaji hao wawili watalazimika kurudi kwenye klabu zao mama mara tu fainali za Euro 2024 zitakapokamilika, ambapo watakwenda kwenye michuano hiyo ya Ujerumani wakiwa kwenye kikosi cha Ureno.

Hata hivyo, Laporta alisema Barcelona inapambana kwa kila namna kuhakikisha inaendelea kubaki na huduma za wachezaji hao kwa ajili ya msimu wa 2024-25 na lengo kubwa ni kuwaomba tena kwa mkopo kutokana na timu kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi.

Felix amekuwa akisakwa na timu nyingi kubwa Ulaya ikiwamo Manchester United ambayo nayo inasuka kikosi chake upya kwa ajili ya msimu ujao.

Barcelona inayokabiliwa na ukata itakuwa na mtihani mkubwa wa kuwabakisha mastaa hao msimu ujao na kuna kila dalili wakaondoka.

BEKI na nahodha wa Real Madrid, Nacho 34, anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa timu hiyo kabla ya wiki hii kumalizika kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo kwa muda mrefu zaidi. Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na kuna uwezekano akasaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

Manchester United imepanga kufanya mazungumzo na wawakilishi wa winga wao, Jadon Sancho dirisha lijalo la majira ya kiangazi kabla ya kuamua juu ya hatma yake. Sancho aliyekuwa akicheza kwa mkopo wa nusu msimu Borussia Dortmund anadaiwa kuwa hana mpango wakuendelea kusalia Man United kwa msimu ujao na badala yake anataka kusaini mkataba wa kudumu na Dortmund.

KIUNGO mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, 21, amesisitiza bado hajafikia uamuzi wa hatma yake na kwa sasa anapambana kwa ajili ya kujiweka sawa kucheza michuano ya Euro. Wirtz ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha Leverkusen katika msimu uliopita ambapo aliisaidia kuchukua ubingwa wa Bundesliga.

STRAIKA wa Manchester City na Argentina Julian Alvarez, 24, ameingia kwenye rada za Atletico Madrid ambayo inafikiria kumnunua mazima au hata kwa mkopo. Alvarez mwenye umri wa miaka 24 amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man City, hivyo amevutiwa na ofa ya Atletico na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali ni hataki kupoteza nafasi hiyo.

KIPA wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga anatarajia kufanya kikao na kocha mpya wa Chelsea Enzo Maresca kujadili hatma yake msimu ujao. Kepa ambaye msimu uliomalizika alikuwa akicheza kwa mkopo Real Madrid, anahitaji kurudi London kupambania namba kikosi cha kwanza baada ya Madrid kuweka wazi hawana mpango wa kumsainisha mkataba wa kudumu badala yake wanataka kumsainisha mkataba wa msimu mmoja.

NAPOLI imeiambia Arsenal kama itakuwa tayari kumruhusu straika wao Victor Osimhen aende kujiunga na miamba hiyo ya Emirates kama tu itaweka ubaoni wachezaji wawili kwenye dili hilo. Osimhen anahusishwa na mpango wa kuachana na Napoli kwenye dirisha hili na Arsenal wanatajwa kuhitaji sana huduma yake.

Atalanta ipo Tayari kumuuza staa wao Teun Koopmeiners dirisha hili kwenda Juventus iliyowasilisha ofa inayofikia Euro 40 milioni. Teun ambaye amekuwa kwenye rada za Liverpool kwa muda mrefu, anahitajika na vigogo kutokana na kuwango bora alichoonyesha msimu uliomalizika akiipa Atalanta ubingwa wa Europa League.