Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi kubwa Man United afunguka

BOSI Pict

Muktasari:

Bosi huyo alisema jambo hilo lina changamoto nyingi, lakini inawezekana kuona Man United kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England hadi kufikia 2028.

MANCHESTER, ENGLAND: MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Manchester United, Omar Berrada amefunguka huku akisisitiza miamba hiyo ya Old Trafford itarejea kwenye kilele cha Ligi Kuu England kufikia 2028.

Bosi huyo alisema jambo hilo lina changamoto nyingi, lakini inawezekana kuona Man United kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England hadi kufikia 2028.

Na kama hilo litahitaji kuwa kweli, basi Man United itahitaji kufanya usajili wa maana kwenye dirisha hili ili kukifumua kikosi hicho kilichomaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi msimu uliopita.

Tayari miamba hiyo imeshamsajili Matheus Cunha kwa ada ya Pauni 62.5 milioni kutoka Wolves, huku ikiwaweka kwenye rada mafowadi wengine akiwamo mkali wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike na staa wa Brentford, Bryan Mbeumo sambamba na straika wa Sporting CP, Viktor Gyokeres.

Lakini, Man United pia itahitaji kufungulia mlango wa kutokea mastaa kadhaa, ikiwamo mawinga watatu Marcus Rashford, Antony na Alejandro Garnacho na wachezaji wengine kadhaa ili kumpa nafasi kocha Ruben Amorim kuwa na kikosi anachokitaka kabla ya dirisha kufungwa Septemba Mosi.

Hadi sasa tayari Man United imeshafanya usajili wa wachezaji wawili, Cunha na beki wa kushoto, kinda Diego Leon kutoka Cerro Porteno, ambaye usajili wake ulithibitishwa Januari na alikuwa anasubiri kujiunga sasa.

Wachezaji wengine ambao wanaweza kuondoka ni Christian Eriksen, Jonny Evans na Victor Lindelof wale wa kikosi cha kwanza na makinda Hubert Graczyk, Jack Kingdon, Sam Murray, Tom Myles, James Nolan na Tom Wooster huku kwenye orodha hiyo inaweza kumhusu pia mmoja kati ya washambuliaji wawili Rasmus Hojlund au Joshua Zirkzee.

Man United ipo tayari kuondoa wachezaji hao ikiamini inaweza kupata huduma ya straika na mawinga wengine, ambapo sasa inamsaka Mbeumo inayemgombania na Tottenham Hotspur na Ekitike na Gyokeres, ambao pia wapo kwenye rada za timu nyingine ikiwamo Arsenal.