Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag amtaka Grealish pale kwa Wirtz

TEN Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa Manchester City na England, Grealish amekubaliana na hali halisi nyakati zake za kutamba Etihad zimefika ukomo na huenda akatimkia zake Ujerumani dirisha hili.

MUNICH, UJERUMANI: STAA ghali Manchester City, Jack Grealish ameripotiwa kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wanaweza kunaswa ili wakachukue mikoba ya Florian Wirtz huko Bayer Leverkusen.

Nyota huyo wa Manchester City na England, Grealish amekubaliana na hali halisi nyakati zake za kutamba Etihad zimefika ukomo na huenda akatimkia zake Ujerumani dirisha hili.

Tottenham, Newcastle na klabu yake ya zamani ya Aston Villa zilikuwa miongoni mwa timu zilizoripotiwa kuhitaji huduma ya mchezaji huyo. Mabingwa wa Italia, Napoli nao waliingia kwenye mchakato wa kunasa saini yake na Kocha Antonio Conte anasaka wachezaji wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Sasa miamba ya Ujerumani, Bayer Leverkusen imeingia kwenye vita ya kumsaka kiungo huyo mshambuliaji, ambaye klabu yake ya Man City inahitaji ilipwe Pauni 40 milioni tu.

Kocha mpya wa Bayer Leverkusen, Erik ten Hag ameripotiwa kuvutiwa sana na Grealish na amewaambia mabosi wa timu hiyo staa huyo ni mtu mwafaka kwenda kuchukua mikoba ya Wirtz.

Wirtz, 22, anajiandaa kujiunga na Liverpool dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi licha ya ofa ya awali ya miamba hiyo ya Anfield ya Pauni 113 milioni kukataliwa wiki iliyopita.

Mkwanja atakaouzwa Wirtz utampa Ten Hag nguvu kubwa kwenye usajili wa mastaa anaowataka dirisha hili na baada ya kumnasa kipa wa Brentford, Mark Flekken, sasa anamhitaji Grealish, ambaye aliigharimu Man City, Pauni 100 milioni wakati ilipomsajili kutoka Villa Park.

MAVITU WA STAA WA PAUNI 100M MSIMU WA 2024-25 KWENYE EPL

-Amecheza: Mechi 20

-Ametengeneza: Nafasi 24

-Amepiga: Pasi 412

-Amefunga: Bao 1

-Ametoa: Asisti 1

-Amepiga: Rafu 5