Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zawadi ya Barker Simba


LICHA ya Simba kukosa ubingwa wa Ligi Kuu NBC msimu huu, Kocha Mkuu, Steve Barker amewashusha presha mashabiki wa klabu hiyo kuwa wana nafasi ya mwisho kuthibitisha ubora na kumaliza msimu kwa heshima pamoja na kutwaa taji.


Kocha Barker ameitoa kauli hiyo wakati Simba ikijianda na mchezo wa  fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Azam FC, itakaochezwa keshokutwa Jumamosi, Julai 4, 2026, kwenye Uwanja wa Gombani, Kisiwani Pemba, Zanzibar.

Raia huyo wa Afrika Kusini, amesema Kombe la Shirikisho la CRDB ndio taji linaloweza kuamua namna msimu utakavyohitimishwa.

Barker amesisitiza kwa sasa nguvu zote zimeelekezwa kwenye fainali ya CRDB Cup, akisema ushindi katika mchezo huo unaweza kubadilisha taswira ya msimu mzima, hasa baada ya kutwaa Kombe la Muungano, hivyo kuongeza taji jingine litakuwa zawadi muhimu kwa mashabiki waliounga mkono timu hiyo msimu mzima.

Amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu katika mchezo huo muhimu, akiahidi kuwa wachezaji wataingia uwanjani kupambana kwa kila namna kuhakikisha taji hilo linarejea Msimbazi.

“Kila mara nimekuwa nikisema tutatoa asilimia 100 kila tunapovaa jezi ya Simba. Hilo halitabadilika kwenye fainali. Tunataka kuwaletea furaha mashabiki wetu kwa kushinda taji na kumaliza msimu kwa tabasamu,” alisema Barker.

Simba ilitinga fainali hiyo kufuatia kuichapa Coastal Union ya Tanga mabao 4-0 huku Azam ikiivua ubingwa wa michuano hiyo, Yanga kufuatia kuichapa kwa mabao 3-2 ndani ya dakika 120 huku ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja.

Katika hatua nyingine Barker alisema licha ya kushindwa kutwaa ubingwa wa ligi, msimu huu Simba imeweka msingi imara wa mafanikio ya baadaye huku kikosi chake kikiendelea kuonyesha ukuaji mkubwa, nidhamu na kujenga mfumo wa uchezaji unaoweza kuifanya timu hiyo kuwa tishio katika misimu ijayo.

Barker alisema Simba ilipambana hadi mwisho katika mbio za ubingwa, ikimaliza msimu kwa ushindi wa mechi 10 mfululizo, hali iliyoiweka presha kubwa kwa Yanga ambao hatimaye walifanikiwa kutwaa taji hilo kwa tofauti ya pointi mbili.

Hata hivyo, kocha huyo amesisitiza kuwa wapinzani wao walistahili pongezi kwa kuhimili presha hiyo kubwa ya mwisho wa msimu.

“Kile tulichoweza kukidhibiti ni kushinda mechi zetu na hilo tulilifanya vizuri sana. Tulimaliza msimu kwa nguvu kubwa, tukashinda mechi 10 mfululizo na tukaendelea kuiweka presha kwa Yanga. Wao walihimili presha hiyo na wanastahili pongezi kwa kutwaa ubingwa,” alisema Barker.

Kocha huyo alisema jambo linalompa matumaini zaidi si matokeo ya ligi pekee, bali mabadiliko ya kiutendaji ndani ya kikosi chake, akibainisha kuwa wachezaji sasa wanaelewa vyema falsafa yake na wameanza kujenga utambulisho wa timu.

Kwa mujibu wake, maendeleo hayo ni msingi muhimu kuliko matokeo ya muda mfupi, akisisitiza kuwa Simba ipo kwenye njia sahihi ya kurejea kileleni.