Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs kumchukua Frank wa Brentford

SPURS Pict

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni mazungumzo yalifanyika wikiendi iliyopita na kocha huyo wa Brentford anakaribia kwenda kuchukua mikoba ya Ange Postecoglou.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Thomas Frank ameripotiwa kukubali kwenda kuwa kocha mpya wa Tottenham Hotspur.

Kinachoelezwa ni mazungumzo yalifanyika wikiendi iliyopita na kocha huyo wa Brentford anakaribia kwenda kuchukua mikoba ya Ange Postecoglou.

Frank, 51, anataka kwenda kuungana na Spurs na kuachana na Brentford baada ya miaka saba. Na sasa kazi imebaki kwa mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy kulipa fidia ya kuvunja mkataba wa kocha huyo huko G-Tech Stadium. Spurs ilimfuta kazi Postecoglou, Ijumaa iliyopita licha ya kocha huyo kuwasaidia kumaliza ukame wa miaka 17 ya kutoshinda taji lolote baada ya kunyakua Europa League mwezi uliopita.

Na Levy anataka huduma ya kocha huyo wa Denmark, ambaye aliongoza Brentford kumaliza nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu.

Kocha wa Fulham, Marco Silva na Bournemouth, Andoni Iraola walikuwa kwenye mchakato wa kusakwa na Spurs, lakini Frank anajiandaa kuwa kocha wa nne wa kudumu wa kikosi hicho katika kipindi cha miaka minne. Frank alijiunga na Brentford mwaka 2018 na baada ya kupanda daraja miaka mitatu baadaye, aliifanya timu hiyo kuwa tishio kwenye Ligi Kuu England.

Kocha huyo tayari anataka kumsajili Bryan Mbeumo, 25, ili wakapige mzigo wote huko Spours, akijaribu kuvamia dili la Manchester United la kumtaka winga huyo Mcamerooni.

Jambo hilo linaweza kumgharimu Levy hadi Pauni 70 milioni, ikiwamo Pauni 10 milioni ya kulipa fidia ya kuvunja mkataba wa Frank na Pauni 60 milioni ya kunasa huduma ya Mbuemo.

Spurs ipo kwenye mtihani zaidi kwa sababu Mbeumo anaweza kuhitaji mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki, ambao utamfanya awe mchezaji anayelipwa kibosi zaidi kwenye kikosi hicho cha London.