Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot anahitaji mshambuliaji Liverpool

MSHAMBULIAJI Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa tovuti ya The Mirror, Liverpool itakuwa na bajeti nzuri itakayowawezesha kufanya usajili wa kishindo katika dirisha lijalo kuhakikisha inaendelea kulitetea taji lao.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL wamepanga kusajili mshambuliaji katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa ndio kipaumbele cha kwanza cha kocha wa timu hiyo Arne Slot.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Mirror, Liverpool itakuwa na bajeti nzuri itakayowawezesha kufanya usajili wa kishindo katika dirisha lijalo kuhakikisha inaendelea kulitetea taji lao.

Ripoti zinaeleza, Slot tayari ameshawasilisha mapendekezo yake kwenda bodi ya Liverpool na wanatarajiwa kufanya kikao baada ya msimu kumalizika.

Hata hivyo, gazeti la Daily Mail linaripoti kwamba majogoo hao hawana mpango wa kufanya sajili zitakazovunja rekodi ingawa watakuwa na bajeti iliyoshiba.

Katika nafasi ya mshambuliaji, ndio eneo la kwanza ambalo timu hii imepanga kuliangalia na sababu za kutaka kuanza kusajili hapo ni kocha Slot kutoridhishwa na kiwango cha Darwin Nunez, wakati Diogo Jota akiwa anaandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Mara kadhaa kocha huyu alikuwa akimtumia Luis Diaz, lakini staa huyu anaonekana kuwa bora zaidi akicheza kama winga kuliko namba tisa.

Baada ya Mohamed Salah kufunga mabao 33 na kuendelea kuwa chanzo cha mashambulizi msimu huu, Daily Mail linaongeza kuwa Slot anataka mshambuliaji wa kati ambaye atamsaidia staa huyu ili pale anapokuwa anapitia kipindi cha ukame timu isiwe inahaha.

"Liverpool wanataka mshambuliaji hilo ni jambo la uhakika kabisa. Pia wana kipaumbele cha kusajili beki wa kushoto, zaidi ya hapo, wanaweza pia kuangalia beki wa kati, kiungo na winga wa pembeni kutegemeana na nani ataondoka."

Liverpool tayari wamefanikiwa kuwapa mikataba mipya Mohamed Salah na nahodha Virgil van Dijk. Hii imewawezesha kuhamasisha nguvu zao kwenye usajili malizika mwisho wa msimu huu.