Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim asema jambo kuhusu Gyokeres

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Amorim anakabiliwa na jukumu kubwa la kujenga upya kikosi cha Man United baada ya kumrithi Erik ten Hag mapema msimu huu, lakini bado hajafanikiwa kubadili mwenendo mbaya wa timu hiyo.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, ametoa maoni yake kuhusu uwezekano wa kumsajili Viktor Gyokeres katika majira ya kiangazi, akisisitiza kwamba staa huyo huenda asijiunge nao.

Amorim anakabiliwa na jukumu kubwa la kujenga upya kikosi cha Man United baada ya kumrithi Erik ten Hag mapema msimu huu, lakini bado hajafanikiwa kubadili mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Ingawa wako kwenye hatua ya nusu fainali ya Europa League, Man United inashikilia nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, na inaweza kumaliza hadi katika nafasi ya 17, ikiendelea kufanya vibaya katika mechi zilizosalia.

Hata hivyo, bado inaweza kufuzu kwa ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao iwapo itatwaa ubingwa wa Europa League.

Kuelekea msimu ujao, Amorim anataka kufanya maboresho ya kikosi chake kwa kusajili mastaa wapya ambao wanaweza kumsaidia na mmoja kati ya hao ni Viktor Gyokeres kutoka Sporting Lisbon anayetajwa sana na vyombo vya habari barani Ulaya.

Kabla ya mechi ya nusu fainali ya Europa League dhidi ya Athletico Bilbao Alhamisi jana, Amorim ambaye hadi sasa amefanikiwa kumsajili Patrick Dorgu tu, aliulizwa kama anaweza kumsajili Gyokeres akajibu: "Sijazungumza naye. Lakini kama mchezaji anataka kujiunga na Man United kwa sababu ya kucheza Ligi ya Mabingwa pekee, basi hawezi kuja. Tunataka wachezaji wanaotaka kuiwakilisha Man United, siyo wale wanaotaka kushiriki mashindano fulani tu."

Kauli hizi za Amorim zinakuja wakati kukiwa na tetesi kwamba Gyokeres anataka kujiunga na klabu itakayocheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Hiyo imesababisha ahusishwe na timu kama Arsenal na kwa mujibu wa gazeti la Ureno A Bola, staa huyo ambaye amefunga mabao 52 msimu huu na jumla ya mabao 95 katika mechi 98 tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Lisbon, anaweza kupatikana kwa Pauni 60 milioni tu.

Arsenal wametajwa kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili Gyokeres, 26, wakihitaji mshambuliaji atakayewasaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kuwa na mapungufu katika eneo hilo hususani kwa msimu huu.