Slot afunguka ishu ya Salah

Muktasari:
- Mshambuliaji huyo raia wa Misri alileta mshangao mkubwa kwenye soka Jumatatu aliposema kuwa hadi sasa hajapewa ofa mkataba mpya mezani, huku ule wa sasa unaomwezesha kukunja Pauni 350,000 kwa wiki ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.
LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amesema mahojiano ya hivi karibuni ya staa wake Mohamed Salah aliyesema hadi sasa hakuna mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya hayajaathiri chochote katika utendaji wa timu na kwa mchezaji huyo.
Mshambuliaji huyo raia wa Misri alileta mshangao mkubwa kwenye soka Jumatatu aliposema kuwa hadi sasa hajapewa ofa mkataba mpya mezani, huku ule wa sasa unaomwezesha kukunja Pauni 350,000 kwa wiki ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.
Salah alisema kwamba yuko “zaidi nje kuliko ndani”, lakini Slot alisisitiza kwamba hali hiyo ya kutokuwa na uhakika juu ya hatma yake inamfanya mchezaji huyo kuwa bora zaidi.
“Sidhani kama hii inamchanganya Mo kabisa, naona kama inamfanya awe bora zaidi ukiangalia kile alichokifanya hadi sasa. Ukichunguza orodha yangu ya wachezaji ninaowachezesha, Mo yuko zaidi ndani kuliko nje. haya mambo ya tetesi na kuzungumziwa na mashabiki na wanahabari ni jambo ambalo ni la kawaida kabisa, na hata katika kiwanja cha mazoezi hakuna mchezaji yoyote aliyekuwa anazungumzia hilo,”alisema Slot.
“Siidhani kama kuna inamsumbua yeye, wachezaji wenzake au mimi, kwa sababu tumeendelea na utaratibu wetu wa kawaida na sikukaa hata kidogo na Mo kuzungumzia suala hilo. Mimi ukiona nazungumza na mo ni kwa sababu ya kumwambia kile ninachokitegemea kutoka kwake, kama ninavyofanya kwa wachezaji wengine wote, kiufupi sijachanganyikiwa na kile alichozungumza na hata wachezaji wenzake pia hawajachanganyikiwa, ni vizuri pia mchezaji kuzungumziwa katika vyombo vya habari kwa sababu hata ninyi(waandishi), mmepata kitu sasa.”