Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi bado mbichi... Rekodi zaibeba Simba

REKODI Pict

Muktasari:

  • Mabao ya dakika 15 za kwanza ya Berkane kwenye Uwanja wa Manispaa ya mji wa Berkane, yaliiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kubeba taji kwa mara ya tatu, lakini Fadlu ametamba mechi ijayo itakuwa tofauti, huku rekodi ya Simba nyumbani ikiibeba dhidi ya Berkane ugenini ikimpa matumaini.

SIMBA imepoteza kwa mabao 2-0 juzi usiku katika pambano la kwanza la fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mbele ya RS Berkane ikiwa ugenini, huku kilichoiangusha kikibainika, lakini kocha Fadlu David amesema mechi haijaisha kwani watajipanga kupindua meza nyumbani.

Mabao ya dakika 15 za kwanza ya Berkane kwenye Uwanja wa Manispaa ya mji wa Berkane, yaliiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kubeba taji kwa mara ya tatu, lakini Fadlu ametamba mechi ijayo itakuwa tofauti, huku rekodi ya Simba nyumbani ikiibeba dhidi ya Berkane ugenini ikimpa matumaini.


SHIDA ILIANZA HAPA

Kabla ya mechi ya juzi, Fadlu aliwaonya wachezaji akiwataka wawe makini na kujihadhari dhidi ya Berkane hasa dakika 20 za kwanza, lakini mastaa hao ni kama hawakuzingatia vizuri na ndani muda uleule aliowatahadharisha walijikuta wakifungwa mabao mawili.

Dosari kadhaa zilionekana na kuchangia Simba kuruhusu mabao hayo, ni wachezaji kupoteza mipira maeneo hatarishi jambo lililowapa fursa Berkane kuwaadhibu na kumaliza mechi mapema.

Kulionekana kama baadhi ya nyota wa Simba hasa wa safu ya ulinzi walianza bila ya kujiamini na hilo likasababisha wakose utulivu walipokuwa na mpira na kujiweka katika ugumu zaidi pale mstari wa mbele wa Berkane ulipowafuata kwa kasi na nguvu ili kuwatengenezea presha.

Udhaifu mwingine wa Simba ulikuwa ni kuachia mianya mingi kwa wapinzani, lakini baadhi ya mastaa hawakuwa na msaada kuutafuta mpira pale walipoupoteza au kumilikiwa na RS Berkane, lakini kujaribu mara kwa mara kutengeneza mitego ya kuotea, ilivyovunjwa na safu ya ushambuliaji ya Berkane, iliitesa Simba.


WA KUCHUNGWA

Kwa mechi ya marudiano, Simba inapaswa kujiandaa kikamilifu kukabiliana na baadhi ya nyota wa Berkane ambao kwa kiasi kikubwa walichangia kuiamua mechi ya juzi.

Kiungo mkabaji Msenegal, Mohamed Camara ndiye anaonekana moyo wa Berkane kwa uwezo mkubwa wa kupora mipira na kuichezesha timu.

Camara ameonyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi na kuisukuma timu mbele na ndiye amekuwa akitumika kunyong’onyesha viungo wa timu pinzani, kama ilivyokuwa juzi kwa Simba.

Mwingine anayepaswa kuchungwa ni kiungo mshambuliaji, Yassine Labhiri mwenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho na ana uamuzi wa haraka pindi awapo na mpira.


REKODI INAWABEBA

Licha ya Simba kupoteza 2-0, bado rekodi zinaibeba kwenye uwanja wa nyumbani ikiwa imeshinda mechi zote sita zilizopita kwa msimu huu kuanzia raundi ya pili hadi nusu fainali, lakini rekodi ya kufungika kwa Berkane ugenini ni sababu ya kuifanya mechi iwe bado mbichi.

Kwa mechi za nyumbani, Simba ilianza raundi ya pili kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya, kisha kushinda mechi zote tatu za makundi dhidi ya Bravos ya Angola 1-0, Sfaxien ya Tunisia (2-1) na CS Constantine ya Algeria (2-0), huku robo fainali iliitoa Al Masry ya Misri penalti 4-1 baada ya kuifunga 2-0 na kufanya matokeo ya jumla yawe 2-2 kwani Simba ilipoteza ugenini 2-0.

Katika nusu Simba ilishinda 1-0 kwenye Uwanja wa New Amaan dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini, lakini hata kwa matokeo ya msimu uliopita ikicheza Ligi ya Mabingwa Afruika ilianza na sare ya 1-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia katika mechi ya raundi ya pili.

Katika makundi ilipata sare moja na kushinda mbili, japo ilipoteza 1-0 robo fainali mbele ya Al Ahly ya Misri, lakini hata katika baadhi za kuamua ukiacha zile za robo fainali zote sita za nyuma ilizocheza na ile iliyopasuka nyumbani mbele ya Jwaneng Galaxy, Simba imekuwa ikitakata.

Pia si mara moja Simba ilishapindua matokeo na kusonga mbele katika michuano  ya klabu Afrika, huku hata ikipoteza kwa mabao mawili au zaidi katika mechi ya kwanza za mtoano na kutoboa.

Mwaka 1979, Simba ilifanya maajabu ya kuitupa nje Mufulila Wanderers ya Zambia jumla ya mabao 5-4 baada ya kuanza kwa kufungwa 4-0 nyumbani kisha kwenda kushinda ugenini kwa mabao 5-0.

Msimu huu katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba ilipindua meza kwa Al Masry ya Misri na kupata ushindi wa mikwaju ya penalti 4-1, baada ya awali kushinda 2-0 na matokeo kuwa sare ya 2-2 kwani ilipoteza ugenini 2-0.

Katika mechi kadhaa za misimu ya hivi karibuni, Simba imekuwa ikipata matokeo mazuri nyumbani, licha ya kupoteza ugenini ikiwamo ile ya 2018-2019 dhidi ya Nkana ya Zambia iliyolala 2-1 ugenini kisha kushinda 3-1 nyumbani na Wekundu kutinga makundi baada ya kupita kipindi kirefu.

Lakini Berkane imepoteza mechi moja ugenini dhidi ya CS Constantine na imetoka pia sare moja msimu huu, licha ya kushinda mechi nne kati ya sita ilizocheza msimu huu katika michuano hiyo ya CAF, kitu kinachotia tumaini kwa Simba itakayokuwa wenyeji Jumapili hii kuanzia saa 10:00 jioni.


FADLU AFUNGUKA

Kocha Fadlu alisema mechi ya marudiano itakayopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa New Amaan, mjini Unguja, itakuwa tofauti na ilivyochezwa ugenini na kwamba kikosi alichonacho kipo tayari kucheza kokote.

“Mechi bado haijaisha na niwatoe hofu wanasimba, mechi ya marudiano itakuwa tofauti na iliyochezwa hapa. Tunaamini nafasi ya kubeba ubingwa wa Afrika ipo na tunaenda kujipanga licha ya kupoteza ugenini,” alisema Fadlu aliyewaka baada ya kusikia mechi inahama kutoka Kwa Mkapa kwenda New Amaan, akisema ni kama wapinzani wao wanabebwa.

“Tuwe wawazi, kucheza Kwa Mkapa unaoingiza mashabiki 60,000 si sawa na kucheza New Amaan, Zanzibar unaoingiza mashabiki 12,000. Bila shaka Simba ni imara inapocheza Mkapa hivyo kuna faida ya kucheza hapo.”