Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simu zimeanza kuita kwa Ruben Amorim

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa, kocha Jose Mourinho yuko katika presha kubwa Benfica baada ya timu hiyo kuwa nyuma kwa pointi 10 katika mbio za ubingwa wa ligi, pia ikishika nafasi ya 25 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LISBON, URENO: SIKU chache baada ya kuondoka Manchester United, kocha Ruben Amorim yupo katika nafasi ya kuajiriwa tena nchini Ureno.

Inaelezwa, kocha Jose Mourinho yuko katika presha kubwa Benfica baada ya timu hiyo kuwa nyuma kwa pointi 10 katika mbio za ubingwa wa ligi, pia ikishika nafasi ya 25 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Gazeti la Daily Mail linadai kuwa Amorim yuko kwenye nafasi nzuri zaidi  ya kuchukua nafasi ya kocha huyo wa zamani wa Man United.

Inaelezwa kuwa nafasi ya Mourinho inaendelea kuwa hatarini, wakati mabosi wa timu hiyo wakiwa tayari wameshaanza mazungumzo na wawakilishi wa Amorim.

AMO 01

Amorim aliwahi kukanusha tetesi za kurejea Benfica Septemba, mwaka jana baada ya mgombea wa urais wa klabu hiyo, Joao Noronha Lopes, kukiri kuwa angependa kumrudisha klabuni hapo.

Lopes pia alienda mbali hata akahudhuria mechi Old Trafford baada ya kuweka wazi kuwa anamwona Amorim kama kocha wa baadaye wa Benfica, lakini mipango yake haikwenda kama alivyotarajia na akashindwa kwenye uchaguzi dhidi ya gwiji wa klabu hiyo, Rui Costa.

Amorim alifukuzwa kazi Manchester United Jumatatu, ikiwa ni baada ya timu hiyo kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Leeds United siku moja nyuma.

AMO 02

Akizungumza baada ya mechi ya Leeds, kocha huyo raia wa Ureno alisisitiza kuwa anataka kuwa meneja kamili, siyo tu kocha mkuu, na alionekana kumkosoa mkurugenzi wa michezo Jason Wilcocks pamoja na mkuu wa usajili, Christopher Vivell.

Inaelezwa maneno hayo yaliwakera sana mabosi hao ambao waliamua kumfukuza Amorim akiwa na rekodi mbaya zaidi ya ushindi ya asilimia 31.9 tu.

Hata hivyo, aliondoka akiwa amelipwa Pauni 12 milioni kama fidia, jambo lililomfanya kuwa kocha aliyelipwa pesa nyingi zaidi baada ya kufukuzwa na Manchester United.

AMO 03

Akizungumzia kuhusu kuondoka kwa Amorim mapema wiki hii,  Mourinho amesema: “Kilichotokea kwa Ruben ni jambo ambalo Ruben mwenyewe pekee ndiye anaweza kulichambua.

“Ninaamini atafanya hivyo, yeye pamoja na benchi lake la ufundi. Kama atafanya hivyo hadharani au la, sijui. Kazi yangu niliyofanya Manchester United ninaifahamu vizuri, na pia najua sababu zilizonifanya niondoke. Lakini kama kawaida yangu, ninapoondoka klabuni hufunga ukurasa na siongelei tena kilichotokea. Sifanyi uchambuzi wa mambo ya ndani. Mlango mmoja unapofungwa, mwingine hufunguliwa. Hivyo ndivyo ilivyotokea nilipoondoka. Historia ilibaki pale, takwimu zilibaki pale, medali tatu zilirudi nyumbani, na hilo ndilo jambo kubwa kwangu.”