Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okello alainisha dili la kiungo Yanga

YANGA imekubali yaishe kwa kumkosa winga Kipre Junior ambaye amerejea klabuni kwake lakini sasa kiungo wao Allan Okello amewalainishia dili la kumpata kiungo mmoja fundi raia wa Uganda.


Unaposoma habari hii tambua kwamba mazungumzo kuhusu usajili wa kiungo Bobosi Byaruhanga anayeichezea klabu ya Oakland Roots kutoka jiji la California  na mabosi wa klabu ya Yanga yanaendelea vizuri ambapo dili hilo linaweza kutimia wakati wowote kutoka na Okello kurahisisha mazungumzo hayo.

Yanga inamtaka Bobosi ambaye ni rafiki mkubwa wa Rais wa Yanga injinia Hersi Said kuja kufanya kazi ndani ya klabu hiyo wakati huu wakisaka kiungo mshambuliaji ambaye anaweza kutokea pembeni au katikati ya uwanja.

Yanga kwenye dili hilo imeshalainishiwa karibu kila kitu na Okello ambaye ameshamaliza kumueleza Bobosi namna maisha yalivyo rahisi ndani ya klabu hiyo kama pande hizo mbili zitafikia makubaliano.

Taarifa kutoka Uganda kwa mmoja wa mastaa wanaoichezea Vipers ni kwamba Okello amepokea simu ya Bobosi akiuliza juu ya maisha ndani ya Yanga baada ya ya kiungo huyo kutafutwa na mabosi wa mabingwa hao wa soka Tanzania.

“Bobosi anaweza kuja Yanga , nimeona anawasiliana na Allan (Okello) akimuuliza namna maisha ya Yanga yalivyo, ametafutwa na viongozi wa Yanga wanataka kumchukua lakini bado hawajamalizana mpaka sasa, alisema mmoja wa mastaa wa Vipers ambaye pia ni rafiki wa Okello.

“Nimemuuliza anasema mazungumzo yao yanakwenda vizuri na yeye Allan amemwambia vizuri kwamba maisha ni mazuri tu hapo Yanga amepokelewa vizuri, wanalipa vizuri na viongozi na mashabiki wanaishi vizuri na wachezaji wao.

Bobosi ndani ya mechi 15 za ya Oakland Roots msimu huu amefanikiwa kutengeneza asisti moja pekee lakini akipata muda wa kutosha wa kucheza, kiungo huyo ambaye ana nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi yake Uganda Cranes.

Yanga imeweka nguvu kwa Bobosi baada ya kumkosa Kipre ambaye amerejea Azam FC mabingwa hao wakimkosa dakika za mwisho kutokana na vipengele vya mkataba kati ya Azam na USM Alger ya nchini Algeria.

Azam iliweka kipengele kwamba kama USM Alger itataka kumuuza kiungo huyo kwa klabu yoyote ya Tanzania basi Azam inapaswa kuulizwa kwanza kwa kupewa kipaumbele kwenye dili hilo na matajiri hao wa Chamazi kumrudisha winga wao huyo wa zamani.