Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SENYO: Kinyozi wa mastaa EPL, anayepiga pesa ndefu

SENYO Pict

Muktasari:

  • Muonekano huo huwa kwa njia nyingi kuanzia mavazi na miili yao kwa ujumla ikiwemo na upande wa nywele.

LONDON, ENGLAND: MBALI ya uwezo wao mkubwa wanaoonyesha kiwanjani moja kati ya mambo ambayo wachezaji wengi wanazingatia ni muonekano wao.

Muonekano huo huwa kwa njia nyingi kuanzia mavazi na miili yao kwa ujumla ikiwemo na upande wa nywele.

Lakini katika nywele, mastaa hawa huwa na machaguo, sio kila mtu anaweza kushika mashine na kuwanyoa, huwa na watu wao maalumu.

Miongoni mwa watu ambao wamepata bahati ya kuwa kinyozi wa wachezaji wengi wa England ni Senyo ambaye amekuwa akihudumia wachezaji wengi wa Jiji la London na nje ya jiji hilo.

Kai Havertz, Bukayo Saka, Bruno Fernandes na Mason Mount ni baadhi tu ya majina maarufu wanayomuita Senyo wanapohitaji kupunguza nywele zao. 

SENY 01

Saluni ya Senyo iitwayo Homme XY ipo kwenye barabara maarufu ya Portabello mjini London na hutumia bidhaa zake mwenyewe za urembo kwa wateja wake. 

Ikiwa mtu yeyote anataka kunyoa tu kawaida katika saluni yake basi itamgharimu Pauni 65 (Sh222,223) wakati huduma ya kufuatwa nyumbani na kinyozi huyu hugharimu Pauni 250 (Sh854,705), ambayo wachezaji wengi huwa wanalipa.

Kabla ya kufungua duka lake mwenyewe, Senyo alikuwa akifanya kazi kwa kinyozi mwingine wa West London, akipunguza nywele za mastaa kama Ryan Bertrand na Scott Sinclair walipokuwa kwenye akademi ya Chelsea. 

Kinyozi huyu amekuwa akinyoa sana wachezaji ambao timu zao zipo ndani ya Jiji la London na wale ambao wapo nje ya Jiji hilo.

Mbali na kutembelea nyumba za wachezaji wa soka, Senyo pia amekuwa akikaribishwa na wachezaji katika kambi zao za kabla ya msimu nchini Marekani, pia aliwahi kwenda Ujerumani wakati England inacheza Euro 2024. 

SENY 02

Legendi wa Chelsea, Ramires, aliwahi kumlipa Senyo asafiri  umbali wa maili 5,500 kutoka London hadi China kila mwezi kwa ajili ya kupunguza nywele baada ya kusaini kwa Jiangsu mwaka 2016. 

Senyo aliiambia SunSport: “Nilikuwa nikipanda ndege kwenda China mara kwa mara wakati Ramires anacheza huko. Hiyo ilikuwa kila wakati. Nilikuwa nikienda walau mara moja kwa mwezi, wakati mwingine mara mbili kwa mwezi. Ilikuwa safari ya siku tatu au nne.”

“Watu hawakuwa wanaelewa kwa wakati huo. Lakini unajua unapokuwa na mtu maalumu anayekunyoa wakati mwingine haiwezekani tu kumpa mtu mwingine yeyote kazi hiyo.

“Ni uhusiano unaojengwa kati yangu na wao, huwa wananipendekeza na kunizungumzia jambo linaloonyesha kwamba mimi ni mtu sahihi.

“Nilimfahamu Ramires kwa sababu msaidizi wake alikuwa akileta mtoto wake apunguzwe nywele, sikujua kama alikuwa ni mtoto wa Ramires kwa wakati huo, siku moja msaidizi huyo aliuliza kama huwa nafanya huduma ya kwenda majumbani. Nilisema, ‘ndiyo, hakuna shida.”

“Nilienda nyumbani kwake na Ramires alifungua mlango. Sikujua kabisa kama nitamuona hapo, tangu wakati huo nilipata bahati ya kuwanyoa mastaa wengine kama Willian na Oscar, nilikuwa na uhusiano mzuri na wachezaji wa Brazil kwa sababu walikuwa wanakaa jirani.” 

SENY 03

Kinyozi huyu pia anasimulia mapito yake kabla ya kufikia hatua hiyo akieleza kwamba alikuwa akifanya kazi mahali ambako wiki nzima alikuwa akipata Pauni 30 tu.

“Hayo ni mambo niliyotakiwa kupitia, ni sehemu ya safari kwa sababu kama ingekuwa rahisi, nisingeweza kuthamini na kujituma hadi kuwa na duka langu mwenyewe.”

Senyo pia alifichua juu ya kile ambacho huwa anazungumza na wachezaji pale anapokuwa anafanya kazi, akisema: “Wako mahali salama, hivyo tunaweza kuzungumza kuhusu chochote tunachotaka, iwe ni familia au jambo lolote. 

“Sio kila wakati ni kuhusu soka lakini wakati mwingine tunatazama soka kwenye televisheni pamoja.” 

Orodha yake ya wateja inaendelea kukua na ndoto yake ni kumpendezesha nywele Cristiano Ronaldo au David Beckham. 

Alisema: “David ni mtu mkubwa. Yeye ni mmoja kati ya watu ambao ningependa kuwahudumia, kitu cha kwanza ninachokiona nikiona mtu yeyote ni nywele zake. Daima huwa nafikiria ni mtindo gani mpya naweza kufanya katika kichwa cha mtu.”