Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Senegal kupiga gwaride la AFCON 2025 Ufaransa

SENEGAL Pict

Muktasari:

  • Senegal iliichapa Morocco kwa bao 1-0 katika fainali ya mashindano hayo mwezi uliopita lakini ushindi huo uliambatana na utata mkubwa.

DAKAR, SENEGAL: MABOSI wa Shirikisho la Soka Senegal (FSF), wanapanga kufanya gwaride la ubingwa Afcon huku nyota wa kikosi cha timu hilo wakiwa na kombe walilolitwaa la Afcon licha ya kuvuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Senegal iliichapa Morocco kwa bao 1-0 katika fainali ya mashindano hayo mwezi uliopita lakini ushindi huo uliambatana na utata mkubwa.

Kocha wa Senegal Pape Thiaw alifanya uamuzi wa kushangaza kwa kuwaondoa wachezaji wake uwanjani baada ya Morocco kupewa penalti katika dakika za mwisho.

Baada ya takribani dakika 10 za kusimama kwa mchezo mechi iliendelea na Brahim Diaz akakosa penalti hiyo jambo lililopelekea mchezo kwenda muda wa ziada ambapo Pape Gueye alifunga bao la ushindi na kuipa Senegal taji lao la pili. Hata hivyo. baadaye Thiaw alifungiwa mechi tano na kutozwa faini ya pauni 72,000 kutokana na tukio hilo la kuwaondoa wachezaji uwanjani.

Mwezi huu, CAF ilitangaza kwa mshangao kuwa Senegal imevuliwa ubingwa huo siku 58 baada ya fainali na Morocco kutangazwa mabingwa wapya.

Shirikisho la Soka la Senegal limeshata rufaa kwenda Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo Duniani (CAS). Rais wa FSF, Abdoulaye Fall amesema kikosi hicho bado kinapanga kuonyesha kombe lao kabla ya mchezo wao ujao dhidi ya Peru leo Jumamosi.

Akizungumza na vyombo vya habari amesema: “Tunachokabiliana nacho ni wizi wa wazi na wa kipekee katika historia ya mchezo wetu. Hatutakubali hali hii. Senegal haitapiga magoti.”

Rais huyo pia ameongeza kwamba wameunda timu ya wataalamu wa kisheria wenye uzoefu mkubwa kupigania haki yao. Ratiba ya timu hiyo kuelekea mechi ya kirafiki imeshatangazwa huku ikijumuisha gwaride la kombe jijini Paris kabla ya mchezo huo utakaochezwa katika dimba la Stade de France.