Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 CAF watujibu maswali haya machache

Muktasari:

  • Kijiweni hapa tumekubali uamuzi wa Kamati kutengua ushindi wa bao 1-0 ambao Senegal waliupata uwanjani na kuwapa Morocco ambao wameupata kupitia email kwa maana baada ya kutuma malalamiko yao.

SAWA Kamati ya Rufaa ya CAF imeipa ubingwa wa AFCON 2025 mezani Morocco baada ya kuamua Senegal ambao awali walikuwa mabingwa walivunja kanuni kwa kutoka nje ya uwanja wakati mchezo unaendelea.

Kijiweni hapa tumekubali uamuzi wa Kamati kutengua ushindi wa bao 1-0 ambao Senegal waliupata uwanjani na kuwapa Morocco ambao wameupata kupitia email kwa maana baada ya kutuma malalamiko yao.

Hata hivyo, pengine CAF wakitujibu baadhi ya maswali tunaweza kuondoshwa kabisa sintofahumu ambayo imegubika vichwa vyetu kutokana na uamuzi huo.

Swali la kwanza ni kwa nini CAF ambayo inaongoza na kusimamia mpira Afrika imeshindwa kuheshimu sheria namba sita ya soka ambayo imempa refa mamlaka ya kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu mchezo.

Mpira ulimalizika kihalali na refa aliamua Senegal imeshinda. Hawaoni uamuzi waliouchukua unaweza kusababisha hadhi na heshima ya waamuzi wa soka Afrika kuporomoka.

Swali la pili ni kama inafahamika kilichofanywa na Senegal kilikuwa ni kosa la kuvunja kanuni, kwa nini mchezo uliruhusiwa kuendea hadi mshindi akapatikana ndani ya muda wa mchezo? Kwamba CAF ilibariki uvunjaji wa kanuni kipindi kile na leo inatoa hukumu kwa jambo ambalo yenyewe ni chanzo pia kwa kukubali mchezo wenye makosa kufanyika.

La mwisho kabisa ni je kama CAF inatambua kanuni hazikufuatwa maana yake maofisa wa mchezo hawakutimiza wajibu wao. Kwa nini walisafishwa na kwa nini hawachukuliwi hatua yoyote?

Wao ndio walikuwa na maamuzi kuhusu mchezo na CAF ikakabidhi kombe na medali kisha ikawasafisha marefa, sasa iweje leo itafsiriwe  kanuni hazikufuatwa?

CAF ikishatupa hayo majibu huenda nyoyo zetu hapa kijiweni zikatulia kwa vile tunaamini matokeo ya soka huwa yanapatikana uwanjani na sio mezani kama ambavyo imetokea katika fainali ya AFCON.