Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mane alia na maamuzi ya CAF akiitaja rushwa

Muktasari:

  •  
  • Mané katika taarifa aliyochapisha katika mitandao ya kijamii leo Jumatano Machi 18, 2026, ameeleza kuwa uamuzi huo unakatisha tamaa na kuua hamasa ya soka.

Mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mané, ameonyesha kusikitishwa na uamuzi wa CAF kuwavua ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco kitendo alichotaja kinaua soka la Afrika huku akidai rushwa imetawala kwenye uamuzi huo.

Mané katika taarifa aliyochapisha katika mitandao ya kijamii leo Jumatano Machi 18, 2026, ameeleza kuwa uamuzi huo unakatisha tamaa na kuua hamasa ya soka.

“Kilichotokea kimezidi. Hii siyo soka tunalolipigania, siyo Afrika tunayoamini,” amesema Mané.

Nyota huyo wa Senegal ameonya kuwa vitendo hivyo vinadhoofisha uadilifu wa mchezo huo na kuharibu uhusiano kati ya soka na mashabiki wake barani Afrika.

“Rushwa imekuwa kubwa mno kwenye mchezo wetu, na inaua hamasa ya mamilioni ya mashabiki. Wachezaji wanajitoa kwa kila hali uwanjani, lakini maamuzi ya nje ndiyo yanaamua mechi na mataji,” amesema na kuongeza,
“Nimesikitishwa si kwa Senegal pekee, bali kwa soka la Afrika kwa ujumla. Tunastahili bora zaidi. Mashabiki wanastahili haki, uwazi na heshima”.

Jana Jumanne, Machi 17, 2026, Kamati ya Rufaa ya CAF ilitangaza kuipa Morocco ushindi wa mabao 3-0 wa mechi ya fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Senegal.

Uamuzi huo unafuatia rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF) kuhusu utekelezaji wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON.