Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sancho anukia Bundesliga, Dortmund, Leverkusen zatajwa

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Sancho ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo wa Chelsea msimu huu akiwa amecheza mechi 29 za michuano yote na kufunga mabao mawili, anapewa nafasi kubwa ya kujiunga na Dortmund kutokana na uhusiano mzuri alionao kati yake na mabosi wa timu hiyo.

KIUNGO wa Manchester United, Jadon Sancho, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Chelsea, anataka  kurudi Bundesliga katika dirisha lijalo ambako kuna timu zinahitaji huduma yake ikiwa pamoja na Borussia Dortmund na Bayer Leverkusen.

Sancho ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo wa Chelsea msimu huu akiwa amecheza mechi 29 za michuano yote na kufunga mabao mawili, anapewa nafasi kubwa ya kujiunga na Dortmund kutokana na uhusiano mzuri alionao kati yake na mabosi wa timu hiyo.

Sancho anahusishwa kuondoka kwa sababu Chelsea haina mpango wa kumsainisha mkataba wa kudumu licha ya kiwango chake alichoonyesha.

Mkataba wa sasa wa Sancho unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, Chelsea inasitasita kumsainisha mkataba wa kudumu kwa sababu ya kiasi cha pesa ambacho kinahitajika na Man United.


Tyler Dibling

SOUTHAMPTON wanahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumuuza winga wao raia wa England Tyler Dibling katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo vigogo mbalimbali ikiwa pamoja na Tottenham na Manchester City zinahitaji saini yake.

Dibbling mwenye umri wa miaka 19, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote.


Jarell Quansah

NEWCASTLE wanataka kutuma ofa ya Pauni 30 milioni kwenda Liverpool ili kuipata huduma ya beki wa kati wa miamba hao wa Anfield, Jarell Quansah, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyu raia wa England mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na msimu huu amecheza mechi 22 za michuano yote lakini nyingi kati ya hizo ameingia akitokea benchini.


Alexander Isak

STRAIKA wa Newcastle United na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak, 25, amekataa ofa ya awali kutoka kwa mabosi wa timu hiyo waliyomwekea mezani ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Mabosi wa Newcastle wanataka kumsainisha fundi huyu mkataba mpya baada ya kuona timu nyingi kubwa zinahitaji kumsajili.



Antoine Semenyo

MABOSI wa Bournemouth watakuwa na kikao kabla ya wiki hii kuisha kujadili mustakabali wa mastaa wao mbalimbali akiwamo beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Hungary mwenye umri wa miaka 21, Milos Kerkez, na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, mwenye umri wa miaka 25.

Mastaa hawa wanawindwa na vigogo mbalimbali barani Ulaya kutokana na viwango vyao.


Neco Williams

NOTTINGHAM Forest wanapambana kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya beki wao wa kushoto anayeichezea timu ya taifa ya Wales,  Neco Williams, 23, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu ujao.

Neco ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Nottingham na msimu huu amecheza mechi 29 za michuano yote.


Dean Huijsen

CHELSEA wameingia katika vita dhidi ya Real Madrid kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto wa Bournemouth na timu ya taifa ya Hispania ambaye ana asili ya Uholanzi, Dean Huijsen, 19. Mkataba wa Dean unatarajiwa kumalizika mwaka 2030. Alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Hispania, Machi 20.


Chris Rigg

KIUNGO wa Sunderland na timu ya taifa ya England kwa vijana wenye umri chini ya miaka 19, Chris Rigg, 17, anafuatiliwa kwa karibu na timu kadhaa za Ligi Kuu England ikiwa pamoja na  Everton, Tottenham na West Ham ambazo zimepanga kumsajili katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka huu.Mkataba wa sasa wa Chris unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.