Samatta, Mo Salah walivyozibeba Tanzania, Misri Ligi Kuu England

Muktasari:
- Inaelezwa mataifa 126 yamewakilishwa na wachezaji wao na yapo yaliyotoa wachezaji wengi na mengine wachache kama ilivyo kwa Tanzania iliyowakilishwa na mmoja, Mbwana Samatta.
LIGI Kuu England ndiyo ligi pendwa zaidi duniani na imekutanisha mataifa mengi yakiwakilishwa na wachezaji wao.
Inaelezwa mataifa 126 yamewakilishwa na wachezaji wao na yapo yaliyotoa wachezaji wengi na mengine wachache kama ilivyo kwa Tanzania iliyowakilishwa na mmoja, Mbwana Samatta.
Samatta alisajliwa na Aston Villa mwaka 2020 akitokea KRC Genk ya Ubelgiji alipodumu kwa misimu minne kuanzia 2016/20 na kufunga mabao 56 kwenye mechi 144 na alijiunga nayo akitokea TP Mazembe ya DR Congo.
Samatta akiwa mchezaji pekee wa Tanzania kucheza Ligi Kuu England, pia ndiye pekee kucheza michezo 14 katika kikosi cha Aston Villa na ameifungia bao moja. Kwa sasa anakipiga PAOK ya Ugiriki.
Mbali na Samatta, wachezaji kama Mohamed Salah, Emanuel Adebayor, Kevin De Bruyne, Riyad Mehrez na wengine, wameyawakilisha mataiufa yao wakiwa ndio waliocheza mechi nyingi zaidi na jumla yao ni wachezaji 126.
Katika ukurasa wa Instagram wa Ligi Kuu England, umeorodhesha majina ya nchi na wachezaji wao mmoja mmoja aliyecheza mechi nyingi na kuandika;
“Nchi 126 zimewakilishwa katika Ligi Kuu England (Premier League), ili kusherehekea utofauti mkubwa wa ligi hii, tumeangazia mchezaji mwenye mechi nyingi zaidi kutoka kila taifa,” ilisema taarifa hiyo.
Mo Salah anayeongoza kwa ufungaji England akiweka kambani mabao 27 hadi sasa amecheza mechi 294, Haaland mwenye mabao 21, Kelvin De Bruyne akicheza mechi 281.
Nyota wengine ni Riyad Mahrez mechi 284, Pele (3), Victor Wanyama (154), Dylan Kerr (5), David De Gea (415), AbduKodir Khusanov (6), Patson Daka (69) na wengine wengi.