Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saliba awapa mzuka Arsenal

SALIBA Pict

Muktasari:

  • Mfaransa huyo ni mmoja wa mabeki wa kati bora duniani na hilo limemfanya asakwe na klabu kibao ikiwamo Real Madrid na Paris Saint-Germain.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa boli, William Saliba amewapa mashabiki wa Arsenal matumaini makubwa baada ya kufunguka yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya kwenye timu hiyo ili aendelezea mapambano ya kusaka taji la ubingwa wa Ligi Kuu England.

Mfaransa huyo ni mmoja wa mabeki wa kati bora duniani na hilo limemfanya asakwe na klabu kibao ikiwamo Real Madrid na Paris Saint-Germain.

Lakini, Saliba, 23 bado anataka kubaki Arsenal kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha kocha Mikel Arteta kupambania mataji.

Alipoulizwa kama atakuwa tayari kusaini dili jipya, Saliba alisema: “Ndiyo, hakika. Kwa sasa bado ila kuna mazungumzo mazuri baina ya wakala wangu wa klabu. Ngoja tuone.”

Huo utakuwa mwendelezo wa mastaa wa Arsenal kusaini mikataba mpya baada ya pacha wa Saliba kwenye safu ya ulinzi, Gabriel kusaini dili jipya la miaka mitano, Mei mwaka huu. Wengine ni makinda Myles Lewis-Skelly na Ethan Nwaneri ambao wataendelea kubaki kwenye kikosi cha Arsenal kwa muda mrefu sambamba na Bukayo Saka baada ya kusaini mikataba mipya.

Saliba alizungumza baada ya Arsenal kufanya vizuri kwenye mechi zake za kirafiki huko Singapore ilipoichapa Newcastle 3-2 na AC Milan 1-0.

Arsenal inaenda huko Hong Kong, ambako itakipiga na Tottenham, Alhamisi. Saliba alivutiwa pia na Arsenal kufanya usajili wa mastaa wapya sita kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Straika Viktor Gyokeres alijiunga na timu hiyo Jumapili iliyopita na sasa Arsenal imehamishia nguvu kwenye kufukuzia huduma ya winga wa Crystal Palace, Eberechi Eze.