Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brighton yavunja benki kwa Luka Vuskovic

LUKA Pict

Muktasari:

  • Beki huyo mwenye umri wa miaka 19 atafanyiwa vipimo vya afya mara baada ya Croatia kumaliza kampeni yake ya Kombe la Dunia.

LONDON, ENGLAND: BRIGHTON imekubaliana na Tottenham Hotspur kumsajili beki wa Croatia, Luka Vuskovic, kwa ada ya rekodi ya klabu ya pauni46 milioni.

Mwezi uliopita, Brighton ilikuwa imetuma ofa mbili kwa ajili ya Vuskovic, lakini zote zilikataliwa.

Hata hivyo, sasa klabu hizo zimefikia makubaliano ya uhamisho huo, ambao pia unajumuisha bonasi zinazoweza kufanya thamani ya jumla ya dili hilo kufikia pauni50 milioni.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 19 atafanyiwa vipimo vya afya mara baada ya Croatia kumaliza kampeni yake ya Kombe la Dunia.

LUK 01

Croatia itacheza dhidi ya Ureno katika hatua ya 32 bora mapema alfajiri ya Ijumaa.

Mzaliwa wa mji wa Split, Vuskovic alikulia katika akademi ya klabu ya Hajduk Split, ambako aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza Ligi Kuu ya Croatia akiwa na miaka 16 pekee. Baadaye pia aliandika historia kwa kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Alikubaliana na Tottenham mwezi Septemba 2023, katika dili lililomruhusu kujiunga rasmi na klabu hiyo mwaka 2025.

LUK 02

Ingawa bado hajacheza mechi yake ya kwanza akiwa na Tottenham, Vuskovic alitumia msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Hamburg ya Ujerumani, ambako alicheza mechi 30 na kufunga mabao sita katika Bundesliga. Kwa sasa anatajwa kuwa mmoja wa mabeki wa kati vijana wanaopewa matumaini makubwa zaidi barani Ulaya.

Brighton imempata Vuskovic kuziba nafasi ya Jan Paul van Hecke katika kikosi cha kocha Fabian Hurzeler.

Cha kushangaza ni kwamba Van Hecke anaelekea Tottenham, baada ya klabu hiyo kukubali kulipa pauni52 milioni kwa ajili ya beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi, ambaye alikuwa amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake na Brighton.