Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rodri kupewa Juve, Mwalimu mzigoni

RODRI Pict

Muktasari:

  • Hiyo ni mechi muhimu kwa timu zote mbili, ambapo Man City inafahamu wazi kitu hamna kingine chochote zaidi ya ushindi ambao utawafanya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi na kupata wakati mgumu wa kukabiliana na Real Madrid kwenye raundi ya 16 bora.

PHILADELPHIA, MAREKANI: KIUNGO, Rodri huenda akarejea uwanjani kuanza kwenye kikosi cha Manchester City kitakachochuana na Juventus katika mechi ya Kombe la Dunia la Klabu, Alhamisi.

Hiyo ni mechi muhimu kwa timu zote mbili, ambapo Man City inafahamu wazi kitu hamna kingine chochote zaidi ya ushindi ambao utawafanya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi na kupata wakati mgumu wa kukabiliana na Real Madrid kwenye raundi ya 16 bora.

Rodri hajaanzishwa kwenye kikosi cha Man City tangu alipopata tatizo la maumivu ya goti, Septemba mwaka jana, lakini kwenye fainali hizo za Marekani alitokea benchini kwenye mechi zote mbili ilizocheza timu yake kwenye hatua ya makundi. Mshindi huyo wa Ballon d’Or alicheza kwa dakika 30 katika mechi hizo mbili na kocha Pep Guardiola sasa anaweza kuamua kumwanzisha.

Mastaa kama Ruben Dias, Phil Foden na Rayan Cherki nao wanaweza kurejea kikosini baada ya kuwekwa benchini kwenye ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Al-Ain. Ilkay Gundogan, aliyefunga mara mbili kwenye mechi hiyo, huenda akakosa mechi ya Alhamisi kutokana na Guardiola kuwa na machaguo mengi ya kufanya kwenye kikosi chake, ambapo Savinho na Jeremy Doku wanatarajiwa kucheza kwenye wingi.

Hata hivyo, mechi hiyo ni fursa kwa mshambuliaji wa Kitanzania, Seleman Mwalimu kuonyesha ubora wake ndani ya uwanja akiwa na kikosi chake cha Wydad, huku mashabiki wa soka la Tanzania watakuwa na fursa ya kumshuhudia pia mkali wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Stephane Aziz Ki akiwa na miamba hiyo ya Morocco.

Mechi zilizopigwa alfajiri, ilizishuhudia Inter Milan ikikipiga na River Plate na Urawa Red Diamonds ilikuwa bize kukwaruzana na Monterrey.