Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid haitaki utani, yatua kwa Cole Palmer

Muktasari:

  • Inaelezwa rais wa Madrid, Florentino Perez ni miongoni mwa viongozi wa Madrid wanaohitaji sana kuona fundi huyu akisajiliwa ingawa changamoto inaonekana kuwa ni bei yake.

MSHAMBULIAJI wa  Chelsea na timu ya taifa ya England, Cole Palmer, 22, ameingia kwenye rada za Real Madrid ambayo inataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Palmer ambaye amekuwa katika kiwango bora tangu ajiunge na Chelsea katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2033.

Inaelezwa rais wa Madrid, Florentino Perez ni miongoni mwa viongozi wa Madrid wanaohitaji sana kuona fundi huyu akisajiliwa ingawa changamoto inaonekana kuwa ni bei yake.

Urefu wa mkataba wa staa huyu unadaiwa kuwa utaigharimu zaidi ya Euro 150 milioni kwa timu yoyote itakayohitaji kumpata.

Vile vile mbali ya bei, Chelsea haionyeshi kuwa na mpango wa kumuuza fundi huyu ambaye msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote na kufunga mabao 11.


WEST Ham imepanga kumsajili straika wa Brighton na Jamhuri ya Ireland, Evan Ferguson, 20, kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji linaloonekana kuchangia mwanzo wao mbaya katika ligi kwa msimu huu. Evan ambaye hajaonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amecheza mechi 12 za michuano yote na kufunga bao moja. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


ARSENAL, Manchester United na Barcelona zinajiandaa kuingia katika vita ya katika dirisha lijalo la majira ya baridi ili kuipata saini ya mshambuliaji wa Lille na Canada, Jonathan David, 24, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu. David anadaiwa kuwa tayari kuondoka na hataki kusaini dili jipya jambo linaloonyesha kuna uwezekano mkubwa vigogo wa Lille kumuuza Januari ili asiondoke bure mwisho wa msimu.


MANCHESTER City inataka kumtoa mshambuliaji mmoja kati ya  Oscar Bobb, 21, au James McAtee, 22, kama sehemu ya ofa kwenda Bayer Leverkusen ili kuipata huduma ya winga wa timu hiyo na Ujerumani, Florian Wirtz ambaye inataka kumsajili katika dirisha lijalo. Mkataba wa sasa wa Wirtz unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Timu nyingi zilitamani kumsajili tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.


KOCHA wa Manchester United yupo tayari kuwaruhusu mastaa wao wawili, kiungo raia wa Denmark Christian Eriksen, 32, na winga wa Brazil, Antony, 24, katika dirisha la majira ya baridi mwakani. Mastaa hawa wanahusishwa kuondoka kwa sababu hawajaonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu hali inayosababisha Ruben Amorim kutaka kuwaondoa ili kusajili mastaa wengine.


MBALI ya Arsenal, Bayer Leverkusen  pia inataka kumsajili kiungo wa Real Madrid na Uturuki, Arda Guler, 19, katika dirisha lijalo la majira ya baridi kwa mkopo wa nusu msimu. Arda ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Madrid msimu huu amekuwa akitajwa kuondoka kwa muda mrefu na hivi karibuni kocha Carlo Ancelotti alisisitiza kuwa bado ana mipango naye.


AC Milan inahitaji kiasi kisichopungua Euro 50 milioni ili kumuuza beki wao wa kushoto, Theo Hernandez, 27, ambaye anawindwa na vigogo mbalimbali barani Ulaya ikiwemo  Manchester United na Real Madrid. Theo ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote na kutoa asisti mbili.


MSHAMBULIAJI wa Atalanta na Nigeria, Ademola Lookman amesisitiza yupo tayari kurudi England anakowindwa na timu mbalimbali ikiwemo Arsenal na Manchester United. Lookman ni mmoja wa mastaa tegemeo Atalanta na mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote na kufunga mabao 10.