Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ratiba EPL yamkera Erik ten Hag

Muktasari:

  • Juzi Man United ilicheza mchezo mwingine wa ligi hiyo dhidi ya Southampton kwenye ushindi wa mabao 3-0 ulioanza saa 6:30 za England sawa na saa 8:30 kwa Afrika Mashariki na amesema mamlaka za soka hazijafanya sawa.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Erik ten Hag amewaka muda waliopangiwa kwenye mechi zao za Ligi Kuu England hawajatendewa haki na zinaathiri kwa kiasi kikubwa matokeo yao uwanjani.

Juzi Man United ilicheza mchezo mwingine wa ligi hiyo dhidi ya Southampton kwenye ushindi wa mabao 3-0 ulioanza saa 6:30 za England sawa na saa 8:30 kwa Afrika Mashariki na amesema mamlaka za soka hazijafanya sawa.

Mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi, Man United ilicheza na Brighton mchezo ulioanza pia saa 6:30 mchana.

Msimu uliopita, mashetani hawa wekundu walicheza mechi tatu za saa 8:00 mchana kwa saa za England, tofauti na msimu huuna mambo yamewabadilikia baada ya kupangiwa mechi za mapema mbili kati ya nne za mwanzoni mwa msimu jambo ambalo liliitokea sana Liverpool ya msimu uliopita chini ya Jurgen Klopp.

Baada ya mchezo dhidi ya Southampton, Man United itasafiri hadi Selhurst Park kucheza dhidi ya Crystal Palace katika mchezo utakaopigwa saa 11:30 jioni sawa na saa 2:30 usiku kwa Afrika Mashariki.

"Kwanza kabisa hii sio sawa, tunapangiwa mechi za ugenini saa 2:00 usiku mechi za saa 6:30 mchana,  haikubaliki lakini kila siku inatukuta, ninajivunia sana mashabiki wetu daima wamekuwa pamoja na sisi hata kwa mechi hizi zinazoonekana ni za mida mibovu, wamekuwa wakifika na kuisapoti timu, hiyo inaonyesha tuna mahusiano mazuri sana," alisema Ten Hag.

"Wanaleta hali nzuri sana tunapokuwa Old Trafford na pia kwenye mechi za ugenini. Nadhani mamlaka za Ligi Kuu zinapaswa kuyapa kipaumbele masilahi ya mashabiki na kuangalia hili suala hili la muda."

Kocha huyo raia wa Uholanzi alipoulizwa pia ikiwa upangaji wa mechi hizo inaathiri uwezo wa timu kiwanjani na kuwapa faida wapinzani alisema:

"Inatuathiri kwa kiasi kikubwa, lakini tunapaswa kukabiliana nalo kama tulivyofanya leo (juzi), timu yetu ipo vizuri lazima tupambane tushinde haijalishi tunapitia changamoto gani, hatuwezi kuleta kisingizio chochote."

Man United ambayo ilipoteza mechi mbili kati ya tatu za mwanzo katika mchezo uliopita ilijipatia ushindi baada ya mabao ya beki wake Matthjis de Ligt na washambuliaji Marcus Rashford na Alejandro Garnacho aliyepachika bao la tatu dakika za lala salama.

Ten Hag anaamini kikosi chake kinazidi kuimarika siku hadi siku kutokana na ilivyocheza kuanzia mechi ya kwanza ya msimu hadi sasa.

"Unaona, katika michezo iliyopita kuanzia Ngao ya Jamii na kuendelea, timu hii inakua, bado inahitaji muda, tunahitaji kujenga timu hii. Tutafika kule tunakohitaji lakini haiwezi kuwa kirahisi hivyo," alisema Ten Hag.