Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford kachangia dili la Sancho Villa

Muktasari:

  • Sancho amejiunga na Aston Villa kwa mkopo wa msimu mzima akitokea Manchester United, wakati Rashford aliichezea klabu hiyo ya Villa Park kwa mkopo msimu uliopita.

BIRMINGHAM, ENGLAND: STAA wa mkopo Aston Villa, Jadon Sancho amefichua kwamba alizungumza na Marcus Rashford kabla ya kukubali uhamisho wa kwenda kukipiga Villa Park katika siku ya mwisho ya dirisha kufungwa.

Sancho amejiunga na Aston Villa kwa mkopo wa msimu mzima akitokea Manchester United, wakati Rashford aliichezea klabu hiyo ya Villa Park kwa mkopo msimu uliopita.

Rashford uhamisho wake ulikuja baada ya kuweka wazi kwamba anataka kwenda kukabiliana na changamoto mpya nje ya Old Trafford. Hakunaswa jumla Villa Park, lakini kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, amekwenda kujiunga kwa mkopo Barcelona huku kukiwa na kipengele cha kumsajili jumla kwa ada ya Pauni 26 milioni itakapofika dirisha la kiangazi mwakani.

Sancho alihusishwa na mpango wa kutimkia Serie A mapema kwenye dirisha ambalo lilifungwa usiku wa Jumatatu wiki hii baada ya kucheza kwa mkopo huko Chelsea msimu uliopita.

Juventus na AS Roma zilihitaji huduma yake kabla ya kuamua kugeukia mawinga wengine.

Na sasa winga huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alisema mazungumzo aliyofanya na Rashford yamechangia katika kufanya uamuzi wa kujiunga na Aston Villa.

“Nilizungumza naye wakati alipokuwa kule msimu uliopita na nafahamu alikuwa anafurahia sana,” alisema Sancho.

“Alizungumza vitu vingi sana vizuri kuhusu klabu, kuwapo kwa mazingira rafiki kwa wachezaji na makocha. Hilo lilinishawishi kwenda.”

Sancho alikuwa mmoja wa wachezaji wanne walioondoka United kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Harry Amass na Rasmus Hojlund nao waliondoka kwa mkopo kujiunga na Sheffield Wednesday na Napoli mtawalia, wakati Antony aliondoka jumla Old Trafford kwenda kujiunga na Real Betis.