Chelsea yamnasa beki Mtaliano
Muktasari:
- Klabu hiyo ya Stamford Bridge ofa yake ya kwanza yenye thamani ya pauni8 milioni ikikataliwa Jumamosi, huku viongozi wa Sunderland wakiona kiwango hicho cha fedha hakilingani na thamani ya mchezaji huyo. Sunderland imesisitiza kuwa nahodha wao mwenye umri wa miaka 33 hauzwi dirisha hili la usajili.
LONDON, ENGLAND: CHELSEA imethibitisha kumsajili beki wa Italia mwenye umri wa miaka 21, Marco Palestra, kutoka Atalanta.
"Ni jambo muhimu kwangu kuwa na Xabi Alonso kama kocha," amesema Palestra, ambaye amesaini mkataba wa miaka sita wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi, katika dili lenye thamani ya takribani pauni48 milioni.
"Nimezungumza naye mara mbili na nina furaha sana kwa sababu aliniambia anachotarajia kutoka kwangu. Ninafurahi kumfahamu na kuanza mazoezi na Chelsea."
Wakati huohuo, Chelsea inapanga kuijaribu Sunderland kwa kuwasilisha ofa ya pili kwa ajili ya nahodha wao, Granit Xhaka.
Klabu hiyo ya Stamford Bridge ofa yake ya kwanza yenye thamani ya pauni8 milioni ikikataliwa Jumamosi, huku viongozi wa Sunderland wakiona kiwango hicho cha fedha hakilingani na thamani ya mchezaji huyo. Sunderland imesisitiza kuwa nahodha wao mwenye umri wa miaka 33 hauzwi dirisha hili la usajili.
Hata hivyo, kutokana na Xhaka kutamani kuungana tena na aliyekuwa kocha wake wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso, Chelsea iko tayari kurejea na ofa nyingine katika jitihada za kumpata kiungo huyo.
Vyanzo mbalimbali havijaweka wazi kiasi cha fedha kitakachokuwa kwenye ofa hiyo ya pili, ingawa Chelsea inaamini kuwa ofa yake ya kwanza ilikuwa ya haki na ilikaribia thamani halisi ya Xhaka.
Nia ya Chelsea kumsajili Xhaka imechochewa kwa kiasi kikubwa na Alonso, ambaye mkataba wake wa miaka minne kama kocha mkuu wa klabu hiyo ulianza rasmi Julai 1.
Alonso na Xhaka walikuwa sehemu ya mafanikio makubwa ya Bayer Leverkusen msimu wa 2023/24, walipoitwaa mataji ya Bundesliga na Kombe la DFB-Pokal. Pia walifika fainali ya Europa Ligi, lakini walipoteza dhidi ya Atalanta.
Sunderland ilimsajili Xhaka kutoka Bayer Leverkusen msimu uliopita kwa ada ya pauni13 milioni pamoja na nyongeza ya hadi pauni4 milioni kulingana na mafanikio mbalimbali.
Akiwa nahodha, aliiongoza Sunderland kufuzu kushiriki michuano ya Ulaya katika msimu wao wa kwanza baada ya kurejea Ligi Kuu ya England, huku akiwa na mkataba unaomalizika mwaka 2028.
Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal, ambaye atatimiza miaka 34 mwezi Septemba, kwa sasa yuko na timu ya taifa ya Uswisi kwenye Kombe la Dunia la mwaka 2026.