Rangnick atinga Old Trafford

Friday December 03 2021
Rang PIC

MANCHESTER, ENGLAND. KOCHA wa mpito wa Manchester United, Ralf Rangnick amefanya ziara ndani ya Uwanja wa Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa wiki iliyopita.

Kocha huyo atakayeinoa Man United kwa muda miezi sita, alionyeshwa sehenu za uwanja huo akiwa sambamba na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo John Murtough.

Rangnick, 63, bado hajaanza kufanya kazi kutokana na masuala ya visa ya kuishi England kuchelewa kukamilika kwa wakati.

Kwa mujibu wa ripoti, kocha huyo huenda akakabidhiwa timu kuelekea mechi inayofuata ya Man United dhidi ya Crystal Palace, itakayochezwa Jumapili.

Kabla ya kutangazwa na kuchukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer aliyefutwa kazi, Rangnick alikuwa mkurugenzi wa maendeleo ya michezo wa klabu ya Lokomotiv Moscow nchini Urusi.

Mjerumani huyo anafahanmika kutokana na uwezo wake kufundisha kwa kutumia mbinu na mifumo mbalimbali, amekubali kuioa Man United kwa muda wa miezi sita.

Advertisement

Man United imeendela kuwa chini ya Michael Carrick akiiongoza timu hiyo tangu mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Villarreal na Chelsea.

Advertisement