Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diogo Jota afariki kwa ajali, gari lawaka moto

JOTA Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Kireno mwenye umri wa miaka 28 alipata ajali hiyo huko Zamora, Hispania, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo.

ZAMORA, HISPANIA: NYOTA wa Liverpool na timu ya taifa ya Ureno, Diogo Jota, ameripotiwa kufariki dunia katika ajali ya gari ikiwa ni siku 10 tu tangu afunge ndoa.


Winga huyo wa Kireno mwenye umri wa miaka 28 alipata ajali hiyo huko Zamora, Hispania, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo.

Ajali hiyo ilitokea katika barabara ya A52, karibu na Manispaa ya Palacios de Sanabria, kwa mujibu wa gazeti la Marca.

Inaripotiwa kuwa katika ajali hiyo, Jota alikuwa pamoja na kaka yake Andre, wakati gari hilo liliachao barabara na kushika moto.
Gazeti la Enfoque linaeleza, kaka yake pia alifariki katika ajali hiyo.

Jota alikuwa anacheza kama winga wa kushoto wa Liverpool, baada ya kujiunga nao akitokea  kutoka Wolverhampton Wanderers mwaka 2020 kwa ada ya Pauni 41 milioni.

Alifunga ndoa siku 10 zilizopita na mpenzi wake, Rute Cardoso na wawili hao walikuwa na watoto watatu kabla ya ndoa hiyo.

Walionekana katika picha ya kufungishwa ndoa wakiwa mbele ya madhabahu pamoja na watoto hao.

Katika maandishi ya picha hiyo ya Instagram waliandika:"Juni 22, 2025. Ndio kwa milele."

Chapisho hilo la Instagram lilipata zaidi ya 190,000 likes na zaidi ya komenti 1,000.

Pia lilijumuisha emoji za moyo kutoka kwa mshambuliaji mwenzake wa Liverpool Darwin Nunez na Natalia Becker, mke wa kipa Alisson Becker.
Katika taarifa iliyotolewa na huduma za dharura za mkoa wa Castilla na Leon, zilisema:

"Chumba cha oparesheni cha 112 Castilla ya Leon kilipokea simu kadhaa zikieleza kuhusu ajali ya gari katika barabara ya A-52, katika Manispaa ya Cernadilla, Zamora.

Gari liliripotiwa lililopita ajali liliwaka moto. Huduma ya 112 iliarifu Polisi wa Barabara wa Zamora, Kikosi cha Zimamoto cha Mkoa wa Zamora, na Kituo cha Uratibu wa Dharura cha Sacyl (CCU) kuhusu ajali hiyo. Kutoka hapo, Kitengo cha Dharura ya Matibabu (UME) na Wahudumu wa Afya wa Huduma ya Msingi kutoka Kituo cha Afya cha Mombuey walitumwa, ambao walithibitisha vifo vya watu wawili katika eneo la tukio."