Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais FIFA... Hili la Senegal lichukuliwe hatua

FIFA Pict

Muktasari:

  • Fainali ya Afcon 2025 iliingia kwenye vurugu mwishoni mwa mchezo pale Thiaw alipowaagiza wachezaji wa Senegal kutoka uwanjani kupinga uamuzi wa refa kuwapa wenyeji Morocco penalti dakika za mwisho.

RABAT, MOROCCO: ISHAKUWA soo. Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya soka (FIFA), Gianni Infantino, amelitaka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuchukua hatua kutokana na kile alichokiita 'matukio mabaya' yaliyojitokeza wakati wa fainali ya AFCON 2025, Jumapili iliyopita huko Rabat, Morocco.

Hilo linakuja wakati kukiwapo na madai Kocha wa Senegal, Pape Thiaw, amesimamishwa kwa muda usiojulikana.

Fainali ya Afcon 2025 iliingia kwenye vurugu mwishoni mwa mchezo pale Thiaw alipowaagiza wachezaji wa Senegal kutoka uwanjani kupinga uamuzi wa refa kuwapa wenyeji Morocco penalti dakika za mwisho.

Beki wa pembeni wa West Ham United, El Hadji Malick Diouf, alihukumiwa kwa kumfanyia faulo Brahim Diaz, hali iliyomfanya mwamuzi Jean-Jacques Ndala kutumia VAR kabla ya kuamuru mkwaju wa penalti katika dakika za majeruhi. Wachezaji wote wa Senegal, isipokuwa gwiji wa Liverpool, Sadio Mane, pamoja na benchi la ufundi, walirejea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa kupinga uamuzi huo.

FIF 01

Baada ya kuchelewa kwa muda mrefu, hatimaye walirejea uwanjani dakika 17 baadaye baada ya Mane kuwataka kurudi kuendelea na mchezo.

Hata hivyo, nafasi ya Morocco kumaliza mechi kwa kishindo ilipotea baada ya mshambuliaji wa Real Madrid, Brahim Diaz kujaribu penalti ya aina ya Panenka, ambayo kipa wa zamani wa Chelsea, Edouard Mendy, aliisoma kwa urahisi na kudaka mpira huo.

Senegal iliendelea kupambana na kufunga bao la ushindi kwenye dakika 30 za ziada shukrani kwa bao la Pape Gueye, ingawa hali ya 'ingekuwaje kama' iliendelea kuwapo.

Katika saa za alfajiri za juzi Jumatatu, Infantino alitumia ukurasa wake binafsi wa Instagram kutoa maoni kuhusu tukio hilo lililoshuhudia Senegal wakikataa kwa muda kuendelea na mchezo baada ya penalti tata kutolewa kwa Morocco. Ripoti Afrika zilidai CAF ilianzisha mchakato wa kinidhamu dhidi ya Thiaw na sasa inapendekezwa kuwa amesimamishwa.

Infantino aliandika: “Tulishuhudia matukio yasiyokubalika uwanjani na jukwaani. Tunalaani vikali tabia ya baadhi ya mashabiki pamoja na baadhi ya wachezaji wa Senegal na watu wa benchi la ufundi.

"Haikubaliki kuondoka uwanjani kwa namna hii, pia vurugu hazivumiliki katika michezo yetu hilo si sahihi kabisa. Ni lazima daima tuheshimu maamuzi ya waamuzi ndani na nje ya uwanja.

"Timu zinapaswa kushindana uwanjani na kwa kuzingatia sheria za mchezo, kwa sababu chochote pungufu ya hapo kinaweka hatarini kiini cha soka lenyewe. Pia ni wajibu wa timu na wachezaji kuonyesha uwajibikaji na kuwa mfano mzuri kwa mashabiki walioko viwanjani na mamilioni wanaotazama duniani kote.

"Matukio mabaya tuliyoyaona leo yanapaswa kulaaniwa na yasirudiwe tena. Nimesisitiza hayana nafasi katika soka na natarajia vyombo husika vya nidhamu vya CAF vitachukua hatua stahiki.”

Tamko la CAF lilisema: “Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linalaani vikali tabia isiyokubalika ya baadhi ya wachezaji na maofisa wakati wa fainali ya TotalEnergies CAF AFCON Morocco 2025 kati ya Morocco na Senegal, iliyochezwa jana (juzi Jumapili) usiku mjini Rabat.

AFA 01

"CAF inalaani vikali tabia yoyote isiyofaa wakati wa mechi, hasa ile inayolenga waamuzi au waandaaji wa mchezo. CAF itapitia picha zote na kuwasilisha kesi kwa mamlaka husika ili hatua zinazofaa zichukuliwe dhidi ya watakaopatikana na hatia.”

Baadaye, kocha wa Senegal, Pape Thiaw alikiri kuwa hakupaswa kuwaagiza wachezaji wake kuondoka uwanjani na kwamba matendo yao hayaiheshimu Afrika.

Amesema: “Hatukukubaliana. Sitaki kurejea kila tukio. Naiomba radhi soka.

"Baada ya kutafakari, niliwaagiza warejee uwanjani. Unaweza kuchukua hatua kwa hasira ya muda. Tunakubali makosa ya mwamuzi. Hatukupaswa kufanya hivyo, lakini imeshatokea na sasa tunaomba radhi kwa soka.”