Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG yaweka mzigo kwa Yamal

Muktasari:

  • PSG imefanya hivyo ikiamini kwamba itafanikiwa katika mpango huo kutokana na Barcelona kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi inayotembea nayo wakati huu ambao soka la Ulaya limeendelea kuwa na gharama kubwa za uendeshaji ikiwamo usajili wa wachezaji.

PARIS, UFARANSA: WINGA wa Barcelona, Lamine Yamal amewekwa kwenye rada ya PSG, ambayo imewasilisha ofa ya Euro 350 ikimtaka nyota huyo msimu ujao akakipige kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1), ukiwa ni mtihani mzito Nou Camp.

PSG imefanya hivyo ikiamini kwamba itafanikiwa katika mpango huo kutokana na Barcelona kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi inayotembea nayo wakati huu ambao soka la Ulaya limeendelea kuwa na gharama kubwa za uendeshaji ikiwamo usajili wa wachezaji.

Linapokuja suala la kuzungumzia kizazi kipya cha wachezaji kwa sasa wanaotawala soka haiwezekani kutomtaja Yamal  anayeng’ara akiitumikia Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, na tangu alipoanza kuonekana kwenye LaLiga akiwa na umri wa miaka 15 alidhihirika wazi kuwa ni kipaji cha kipekee chenye uwezo wa kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani.

Nyota huyo amefikia jambo hilo tayari akiwa na umri wa miaka 18 na tayari ameshateuliwa kuwania Ballon d’Or, ambapo aliangukia katika nafasi ya tatu. Ni kwa sababu hiyo PSG, klabu iliyozoea kubeba nyota wa timu kubwa inafikiria kwa uzito kuweka mezani kiasi hicho kikubwa cha fedha ili kumsajili kinda huyo wa Hispania. Hatua hiyo inakumbusha usajili wa Neymar miaka michache iliyopita, ambapo aliondoka Barcelona na kutua PSG kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia ya Pauni 98 milioni.

Vyombo mbalimbali vya habari vinadai kuwa PSG inaandaa ofa ya takriban Euro 350 milioni, kiasi ambacho hakitaitikisa tu Barcelona, bali soka la Ulaya.

Kwa mujibu wa taarifa, uongozi wa PSG unamuona Yamal kama mhimili mkuu wa mradi wake mpya wa kisoka, hasa baada ya kujidhihirisha kuwa nyota huyo yupo katika kiwango cha juu cha soka la Ulaya kwa sasa.

Euro milioni 350 zinaweza kuonekana kuwa kiasi kisicho halisi, lakini soko la sasa Yamal anastahili thamani hiyo. Takwimu zake zinathibitisha hilo akiwa amecheza zaidi ya mechi 150, akichangia  mabao na asisti zaidi ya 70 zinazomweka miongoni mwa vipaji vinavyoamua matokeo katika kizazi chake.

Hii siyo mara ya kwanza kwa PSG kujaribu kumsajili; waliwahi kutoa ofa ndogo awali ambayo ilikataliwa na Barcelona, lakini safari hii wanaonekana kuwa siriazi zaidi. Kwa Barcelona ingawa imekumbwa na changamoto za kifedha miaka ya karibuni, imeweka wazi kuwa haitamuachia nyota huyo mwenye thamani kubwa zaidi kwa sasa Ulaya, ambaye imemuwekea ada ya takriban Pauni 300 milioni ili kumuuza.